Sunday, 27 June 2010

HAVE YOU EVER VISITED RUAHA NATIONAL PARK? HERE ARE SOME CLUES

Ruaha National Park is the largest national park in Tanzania. Located in the middle of Tanzania about 130 km from Iringa, the park is part of a more extensive ecosystem which includes Rungwa Game Reserve, Usangu Game Reserve, and several other protected areas.
The name of the park is derived from the Great Ruaha River, which flows along its south-eastern margin and is the focus for game-viewing. The park is very rich in both Fauna and flora diversity and can be reached by car via Iringa. There is an airstrip at Msembe, park headquarters. Underhere are some wildlife diversity.
FROM THE MAIN PARK ENTRENCE, THIS IS WHAT YOU SEE


Friday, 11 June 2010

Bajeti ya Kilimo Kwanza

11th June 2010

  • Kodi zake kibao zafutwa
  • Za bia, sigara, magari juu
  • Petroli, dizeli zapona
Bajeti mpya ya mwaka wa fedha wa 2010/11.

Serikali imetangaza bajeti mpya ya mwaka wa fedha wa 2010/11 ambayo imejielekeza kusaidia zaidi wakulima na wafugaji kwa kuwaondolea kodi mbalimbali, lakini imeendelea na jadi yake ya kuongeza kodi kwenye bia, vinywaji baridi, mvinyo, pombe kali, sigara na usajili wa magari.

Akiwasilisha bajeti hiyo bungeji jana jioni, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mukulo, alisema ongezeko la kodi hizo ni la asilimia nane kiwango ambacho hakizidi mfumuko wa bei.

Katika bajeti hiyo, mafuta ya petroli na bidhaa zake zote kodi zake hazijaguwa. Hata hivyo kuna punguzo mafuta ya kuendesha mitambo kutoka Sh. 97 hadi 80 kwa lita.

Ongezeko la viwango hivyo na vile vya zamani kwenye mabano ni vinywaji baridi Sh. 63 kwa lita (Sh. 58) na bia inayotengenezwa na nafaka ya hapa nchini na ambayo haijaoteshwa Sh. 226 kwa lita (Sh. 209) wakati bia nyingine zote zimepanda kutoka Sh. 354 kufikia Sh 382 kwa lita.

Alisema mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25 itakuwa Sh. 1,223 kwa lita (Sh 1,132) na vinywaji vikali itakuwa Sh. 1,812 kwa lita (Sh. 1,678).

Kwa upande wa sigara, Mkulo alisema zile zisizokuwa na kichungi na zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75 itakuwa Sh. 6,209 kwa sigara 1,000 (Sh. 5,749).

Kwa sigara zenye kichungi na zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, itakuwa Sh 14,649 (13,564).

Alisema sigara nyingine zenye sifa tofauti na hizo, itakuwa Sh. 26,604 kwa sigara 1,000 (Sh. 24,633).

Wakati huo tumbaku ambayo ipo tayari kwa utengezaji wa sigara itakuwa Sh. 13,436 kwa kilo (12,441 na ushuru wa cigar unabaki kuwa asilimia 30.

“Hatua hizi katika ushuru wa bidhaa kwa pamoja zinatarajiwa kupunguza mapato ya serikali kwa kiasi cha Sh. bilioni 20.042,” alisema.

Mkulo alisema serikali imesamehe kodi ya majengo kwa nyumba wanamoishi wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60, ambao hali zao kiuchumi haziwawezeshi kulipa kodi hiyo.

“Hata hivyo msamaha huo utatolewa kwa wale watakaothibitishwa na uongozi katika serikali za mitaa kuwa kweli hawana uwezo wa kulipa kodi husika,” alisema.

Pia alisema kiwango cha kutoza ushuru wa mazao shambani kitakuwa kati ya asilimia 3 na 5 ya bei ya kuuza mazao mashambani, ili kuzipa fursa halmashauri na serikali za mitaa kutoza ushuru huo kulingana na uwezo na rasilimali zilizopo.

Ada ya usajili wa magari na pikipiki

Alisema usajili wa magari unatapanda kutoka Sh. 120,000 hadi Sh. 150,000 wakati pikipiki itakuwa Sh. 45,000 ikilinganisha na Sh 35,000 za awali.

Mkulo alisema hatua hizo zitaongeza mapato ya serikali kwa Sh. bilioni 3.19

Ada ya mwaka ya leseni

Kwa upande wa ada ya mwaka ya leseni za magari itakuwa Sh. 50,000 badala ya Sh. 30,000 kwa gari lenye ujazo wa injini 0-500cc.

Gari lenye ujazo wa injini 501 hadi 1,500cc, itapanda kutoka Sh. 50,000 hadi kufikia Sh. 100,000 wakati lenye ujazo wa kati ya 1501-2,500 itakuwa Sh 150,000 badala ya Sh 100,000.

Kwa upande wa gari lenye ujazo wa injini zaidi ya 2,501 ada itakuwa Sh 200,000 badala ya Sh. 150,000 ya sasa.

“Hatua hizi katika kuongeza viwango vya ada ya mwaka ya leseni za magari kwa pamoja zinatarajiwa kuongeza mapato ya serikali kwa kiasi cha Sh. bilioni 16.981,” alisema.

Usafirishaji korosho

Mkulo alisema kutakuwa na ongezeko la ushuru wa kusafirisha korosho ghafi kutoka asilimia 10 ya sasa hadi 15 (ama Dola 160 za Marekani) kwa tani moja.

Alisema lengo la ongezeko hilo ni kulinda viwanda, kuongeza ubora na thamani ya korosho na kukuza ajira kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Mkulo hatua hiyo inatarajiwa kuongeza mapato ya serikali kwa Sh bilioni 2.613.

Michezo ya kuhabatisha

Mkulo alisema kiwango cha kodi inayotozwa kwenye mashine za michezo ya kubahatisha itaongezeka kutoka Sh. 16,000 hadi 32,000 wakati kodi ya kiwango cha asilimia 13 ya mapato itatozwa katika mashine ya tombola, hivyo kuongeza mapato ya serikali kwa Sh. bilioni 0.5.

Misamaha wa kodi

Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika usafirishaji wa mazao ya kilimo kutoka shambani hadi kwenye viwanda vya usindikaji kwa wakulima wenye kilimo cha mkataba wa miwa, mkongwe na chai imesamehewa.

Kodi nyingine iliyosamehewa ni VAT katika mashine na vifaa vya vya kukusanya, kusafirisha na kusindika maziwa ili kuhamasisha uwekezaji katika sekta ndogo ya maziwa na kuboresha kipato kwa wananchi.

Mashine na vifaa vitakavyohusika katika msamaha huo ni vifaa maalum vya kubebea maziwa, pampu maalum za kusukumia maziwa na bomba maalum la kupitishia maziwa kwenye viwanda vya usindikaji.

Vifaa vingine vilivyopata msamaha huo ni kompresa maalum zinazotumika kwenye vifaa vya kupoza maziwa, matanki ya kuhifadhia maziwa gari maalum lenye kifaa cha kupoza na kusafirisha maziwa.

Vingine ni mtambo maalum wa kuchemsha maziwa ili kutoa siagi, vifaa maalum vya kupoza na kutengeneza ubaridi na kifaa maalum cha kukandamiza na kukamua maji ili kuzalisha jibini.

Mkulo alisema msamaha mwingine umetolewa kwenye mashudu kwa ajili ya chakula cha mifugo.

Hatua hiyo inalenga kuhamasisha ufugaji bora na kuwawezesha wakulima wa mbegu za mafuta kupata bei yenye tija kwa mauzo ya bidhaa hiyo.

Pia, serikali imetoa unafuu maalum wa VAT kwa vifaa vinavyouzwa kwa watalaam wa mifugo waliosajiliwa.

Vitu vingine vilivyosamehewa VAT ni zana za kilimo kama kivuna nafaka, pick up balers, mashinde ya kufunga majani ya ng’ombe (hay making machinery) na mowers vinavyotumika mahsusi katika uzalishaji wa kilimo na mifugo.

Sekta ya kilimo cha maua nayo imenufaika na msamaha wa VAT kwa ufarishaji wa maua kwa ndege kwenda nje ya nchi, kwa mabanda (green house) yanayotumika katika kilimo cha maua.

Bajeti hiyo inaonyesha pia kutoa unafuu maalum wa VAT katika uuzaji wa bidhaa na huduma zinazotolewa kwa wakulima waliosajiliwa ama mashamba ya vyama vya ushirika na ujenzi wa miundombinu ya mashamba.

Miundombinu hiyo ni pamoja na mitaro ya umwagiliaji, barabara za mashambani, ujenzi wa maghala au huduma nyingine zinazofanana na hizo.

Pia msamaha wa VAT umetolewa kwa huduma za kuzalisha mifugo kwa njia ya kupandisha mifugo na kutumia mashine maalum za kuzalishia ama kutotolea vifaranga.

Mkulo alisema ili kuhamasisha uwekezaji na uzalishaji katika sekta ya viwanda nchini, unafuu maalum wa VAT umetolewa kwa waendelezaji wa maeneo yenye uwekezaji kwenye bidhaa za kuuza nje yaani EPZ na SEZ.

Mkulo alisema kutakuwa na tozo la VAT kwa asilimia sifuri katika usindikaji na uzalishaji wa mafuta ya kula kwa wazalishaji wanaotumia mbegu za mafuta zinazozalishwa hapa nchini.

Alisema VAT imesamehewa katika vifungashio vya juisi za matunda na bidhaa za maziwa.

“Hatua hii inalenga katika kupunguza gharama za uzalishaji na kuboresha thamani ya bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda vya juisi na maziwa hapa nchini,” alisema.

Mkulo alisema serikali imerejesha utaratibu wa kutambua baadhi ya vifaa kama bidhaa za mtaji kwa wawekezaji ili kuvipa nafuu ya kodi.

Hata hivyo, alisema serikali itaunda kamati maalum ya kushughulikia suala hilo, ili kudhibiti matumizi mabaya ya utaratibu huo yanayoweza kuvujisha mapato.

Alisema hatua hizo zinazohusu VAT zitasababisha kupungua kwa mapato ya serikali kwa kiasi cha Sh. bilioni 2.39.

Kuhusu sheria ya kodi ya mapato sura 332, Mkulo alitoa kauli ya kurekebisha kifungu cha 11 cha sheria hiyo ili kuweka wigo wa ukomo wa maeneo ya uchimbaji wa madini.

Alisema nia ni kudhibiti gharama zinazotakiwa kutolewa katika kukokotoa faida, itakayotozwa kodi ya mapato kwa eneo husika.

Pia kutokana na kuwepo biashara nyingi zinazofanywa na watu wasiokuwa na namba za utambulisho wa mlipa kodi (Tin), alipendekeza kodi ya zuio inayozuiwa na serikali kwa wauzaji wa bidhaa na watoa huduma wasiokuwa na Tin, izuiwe.

Mkulo alitangaza punguzo la ushuru wa bidhaa kwenye mafuta mazito ya kuendesha mitambo kutoka Sh. 97 hadi 80 ili kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa hapa nchini.

Alisema hatua hiyo imezingatia ridhaa ya serikali kukuza viwanda, ajira na mapato ya ndani.

Pia alisema punguzo hilo limezingatia makubaliano ya serikali na wenye viwanda kupunguza ushuru huo na hatimaye kuufuta katika kipindi cha miaka mitatu.

Waziri huyo aliomba Bunge liidhinishe Sh. milioni 11,609,557 kati ya hizo matumizi ya kawaida ni Sh. milioni 7,790,506 na za maendeleo ni Sh. milioni 3,819,051.

CHANZO: NIPASHE