Friday, 31 May 2013

Wabunge nusura watwangane kwa sababu ya hoja ya Mh. Wenje na dhana ya Uliberalia na Ushoja

Mh, wenje

Taarifa ya uchunguzi juu ya kuteswa Kibanda

absalom-kibanda 
Kibanda, ambaye ni Mwenyekiti wa TEF, alitekwa na watu wasiojulikana Machi 5, 2013 mwaka huu na kukumbana na mateso karibu na maeneo ya nyumbani kwake, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Kutokana na hali hiyo, TEF iliamua kuunda timu ya watu watano kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo na viashiria vya kutishia usalama wa wanahabari nchini.
Taarifa hiyo, ambayo pia ilisomwa na Mwenyekiti wa Kamati iliyofanya uchunguzi huo, Deodatus Balile kwenye mkutano wa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari uliofanyika mjini Tanga, imebainisha viashiria mbalimbali vilivyofanya Kibanda kukutana na zahama hiyo.
Pia imevitaka vyombo vya dola kufanyia kazi ripoti hiyo, ili kufuatilia viashiria vilivyoainishwa na wahusika wakamatwe.
Ifuatayo ni ripoti kamili ya uchunguzi:

Thursday, 30 May 2013

Dr. John. P. Magufuri: Sina ubia urais na Sitta 2015

 
Dk John Magufuli 

Dodoma. Siku chache baada ya Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta kumhusisha Dk John Magufuli na kundi la urais la mwaka 2015, Waziri huyo wa Ujenzi, ameibuka na kupinga kauli hiyo, akisisitiza hafikirii kuwania nafasi hiyo.

Habari njema : Serikali yapandisha mishahara sekta binafsi

 
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akijibu hoja za wabunge waliochangia makadirio ya matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2013/14, bungeni Dodoma, jana. 
Picha na Emmanuel Herman  

Dodoma. Wizara ya Kazi na Ajira imetangaza kuongeza mishahara kwa sekta binafsi kwa kati ya asilimia 20 hadi 65, huku ikikusudia kuongeza nafasi za ajira zaidi ya 300,000 kwa mwaka 2013/14 na kujenga mazingira mazuri kwa ajira binafsi kupitia miradi mbalimbali.
Akitoa makadirio ya matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2013/14 jana, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka alisema wizara imekamilisha utafiti na majadiliano ya kima cha chini cha mshaharakatika sekta binafsi 12.

Video ya Mchango wa Mchungaji Msigwa bungeni imekuwa shared 904 times na imekuwa maarufu kule Kenya na nchi za jirani.


Friday, 24 May 2013

Tanzania Mtwara gas riots: 'Pregnant woman killed'


 A house set alight in Mtwara, Tanzania in May 2013
Schools and businesses in Mtwara are closed because of the tensions
A pregnant woman has been shot dead in Tanzania during a security operation after protests in Mtwara, a journalist in the southern town has told the BBC.
The security forces were hunting for those thought to be behind the violent riots that erupted two days ago.
Residents were angered that the budget, presented in parliament on Wednesday, confirmed the construction of a gas pipeline from Mtwara to Dar es Salaam.
They want a gas processing plant to be built in Mtwara instead.
The 500km (310-mile) pipeline is part of a $1.22bn (£807m) project which will also see the construction of a gas processing plant in Dar es Salaam, the main city of the East African nation.
Map
Fleeing Journalist Abdallah Bakari, who works for Tanzania's privately owned Mwananchi newspaper, told the BBC Swahili service that the woman was shot in her home on Thursday.
The security forces were going house-to-house to search for people they thought had been involved in the clashes with police.
Dr Mohamed Kodi at Mtwara's Ligula Referral Hospital told Mwananchi that the woman who died was shot in the stomach. She was seven months pregnant, he said.
Her shooting was also reported in the Kiswahili-language paper Nipache.
The local police commander has refused to comment on the incident.
Correspondents say many men have fled the town because of the crackdown and some women and children have sought shelter in the grounds of Ligula Hospital for safety.

Burning tyres in Mtwara in Tanzania - May 2013 The riots began on Wednesday when the budget confirmed the gas project was going ahead.


When the riots broke out on Wednesday, some buildings and vehicles were set alight, cars were stoned and a bridge blocked to stop traffic.
Riot police were deployed and soldiers can now be seen patrolling the streets.
Police have been escorting buses travelling into Mtwara to stop them being attacked.
Shops, schools and other businesses in the town remain closed because of the tensions.
There were similar protests in January about the proposed pipeline when the houses of several governing party politicians were burnt down.
Parliament has been temporarily suspended because of the latest trouble.
But President Jakaya Kikwete has said the government will continue with the project despite the protests.
Their demands are not valid because resources belong to the whole country, not one geographical area, he said.

Source: BBC.Com

HALI BADO NI TETE MTWARA


Na Waandishi Wetu, Mwananchi  (email the author)

Posted  Alhamisi,Mei23  2013  saa 19:32 PM
Kwa ufupi
Magomeni A hatuna amani, askari wanaingia nyumbani kwetu, wanatupiga na kutunyang’anya simu, yaani huku Magomeni hatuna amani kabisa, tumepotezana na watoto na hatujui hata waume zetu wako wapi


Mtwara. Wakati mtu mwingine akiripotiwa kufa, hali bado ni tete katika Mji wa Mtwara kutokana na mabomu ya machozi na risasi za moto kuendelea kurindima kwenye mitaa kadhaa wakati polisi wakipambana na makundi ya vijana wanaopinga mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mohamedi Kodi alithibitisha kupokea mwili wa mjamzito ukiwa na tundu tumboni, linaloaminika kuwa linatokana na risasi.
“Ni kweli kwa leo tumepokea maiti moja ya mwanamke ambaye ni mjamzito wa miezi saba akiwa amepigwa risasi tumboni,” alisema Dk Kodi. Inadaiwa kwamba mjamzito huyo ambaye jina lake halikufahamika, ameuawa akiwa nyumbani kwake. Kifo hicho ni cha pili baada ya Karim Shaibu (22), mkazi wa Chikongola kuuawa juzi.

WOULD YOU LIKE TO BE A WRITER, AUTHOR OR COLUMNIST. HERE IS YOUR CHANCE

TASAO like other blogs, would like to invite anyone who is inspired in writing different social, cultural, economic and political issues . The most important thing is to ensure your writings does not create any conflict in terms of language used and remember to be sure of what you write and if possible site the source of information for evidence based facts.

It is very easy if you are ready for this motivation. Just write and send to us via our 
Email: studentsunion.oslo@gmail.com
All of your writings will be published here for the readers.
Thanks
PRO

Thursday, 23 May 2013

Askari-watuhumiwa-kubaka-kumwua-mjamzito-kupora-kuchoma-nyumba-moto

Picture
Askari wakiwa lindoni/doriani, Mtwara
Hali ya usalama katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani hapa imezidi kuwa mbaya baada ya askari polisi kudaiwa kufanya unyama kwa kuwabaka wanawake na kumpiga risasi mjamzito

Mbali na unyama huo polisi pia wanadaiwa kuchoma moto nyumba tatu za wananchi katika mtaa wa Magomeni na vibanda vya maduka kadhaa na kupora vitu vilivyomo ndani.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa anasema hali ni shwari na kwamba wananchi watoke nje kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mohamedi Kodi amethibitisha kupokea mwili wa mjamzito ukiwa na tundu tumboni, zinazoaminika kuwa za risasi na hivyo kufanya idadi ya maiti zilizopokelewa hospitalini hapo kufikia mbili na majeruhi 18: “Ni kweli kwa leo tumepokea maiti moja ya mwanamke ambaye ni mjamzito wa
miezi saba, amepigwa risasi tumboni...” “...pia tumepokea mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Chuno, amevunjwa miguu yote kwa risasi.”

Habari zinadai kuwa mjamzito huyo ameuawa akiwa nyumbani kwake baada ya polisi kuvamia makazi yake.

Huduma za kijamii zimesimama, hakuna maduka yaliyo wazi, hakuna usafiri wa daladala wala pikipiki, mji upo kimya, sauti za milio ya mabomu na bunduki zimetawala, wanajeshi waliovalia sare wameuzingira mji wakiwa katika magari na pikipiki.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari kwa nyakati tofauti wakazi hao wamelalamikia kitendo cha askari wa jeshi la polisi kuingia katika makazi yao, kuwapiga, kuwabaka na kuwapora mali zao:

“Magomeni A hatuna amani askari wanaingia majumbani mwetu wanatupiga na kutunyang’anya simu, yani huku Magomeni hatuna amani kabisa, tumepoteza watoto na hatujui hata waume zetu wako wapi” alisema Paulina Idd na kuongeza: “Majumba yetu yamechomwa moto wanaofanya fujo ni polisi wenyewe halafu wanakuja wanatubaka na kuiba mali zetu halafu tunateseka sisi yaani tumechoka kabisa na serikali yenyewe,” alisema Paulina.
Picture
Wanawake na watoto wakiwa hospitali ya rufaa ya Ligula, Mtwara kwa ajili ya kuomba hifadhi baada ya kuyakimbia makazi yao kwa hofu
Kamanda Sinzumwa alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa atapingana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Mchimbi aliyewasili Mtwara leo: “Kuhusiana na suala hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa kwani nitapingana na Waziri wangu kwani leo ametoa tamko bungeni na leo atawasili,” alieleza Sinzumwa

Wakazi wakimbia maeneo yao
Wakazi wa maeneo mbalimbali wamekimbia makazi yao hususani wanawake na watoto na kuhamia hospitali ya rufaa kwa kuhofia usalama wao huku wengi wao wakipotezana na ndugu zao.

Hali hiyo imetokea kufuatia kuwepo kwa milipuko ya mobomu katika maeneo mbalimbali mjini hapa huku huduma za kijamii zikiwa bado zimesitishwa. Hali hiyo imetokea baada ya kusambazwa kwa vipeperushi vilivyokuwa vikihamasisha wananchi wa mkoani hapa kusitisha huduma zote hapo jana  ili kusikiliza hotuba ya wizara ya nishati na madini.

Kufuatia hali hiyo imesababisha kifo kwa raia mmoja aliyefahamika kwa jina Karim Shaibu (22) mkazi wa Chikongola ambaye alipigwa risasi wakati wa fujo kati ya jeshi la polisi na wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari mganga mkuu wa mkoa hospitali ya rufaa ya Ligula Dk Sadun Kabuma alithibitisha kupokea kwa kifo hicho ikiwa ni pamoja na majeruhi 17 wakiwemo askari watatu: “Ni kweli jana kuanzia majira ya saa 10 hadi saa 11 nilipokea majeruhi 17 ambapo kati ya hao wamishtuko ni wanawake watano na askari watatu na kijana mwingine ambaye alikuwa na jeraha na katika harakati zan kumwokoa maisha yake alifariki akiwa chumba cha upasuaji,” alisema Dk Kabuma

Wananchi wazungumzia bajeti

Wakizungumzia uwasilishwaji wa hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini wakazi wa hapa wamesema kuwa hawakubaliani na ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kwani mpango huo utawaletea dhuluma: “Mpango wa kusafirishwa kwa gesi asilia hatuna mpango nao kwa wakazi wote wa Mtwara kwa kifupi akina mama wa mtwara hatutaki itoke,” alisema Fatuma Abdallah.

---
Imenukuliwa kutoka wavuti.com kwa msaada wa KARIBU KUSINI Blog

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/05/mtwara-askari-watuhumiwa-kubaka-kumwua-mjamzito-kupora-kuchoma-nyumba-moto.html#ixzz2U8mSnwWA

Uhuru Day, Easter party, and Muungano PICTURES- Mixed Reactions


TANGAZO MUHIMU

Ndugu wanaTASAo kama ilivyo ada yetu ule muda wa kuwaaga wenzetu wanaomaliza masomo mwaka 2013 umewadia. Sherehe zitafanyika siku ya Jumamosi ya Tarehe 08.06.2013. Sherehe hizi zitafanyika katika Ukumbi wa NORGBERG KIRKE pale ilipofanyika sherehe ya Uhuru mwezi Desemba 2012. Sherehe zitaanza saa 12.00 jioni.

Tunaomba sana wote tushiriki kwa wingi.

Sambamba na hilo tunaomba kuwakumbusha michango ya Kiingilio na Ada ya kila muhula kwa wale ambao hawajatoa. Kwa sababu sherehe hizi zinaendeshwa kwa michango yaani Kiingilio na Ada tu hakuna mchango zaidi ya huo. Tunawaomba sana tujitume wenyewe. Unaweza wasilisha mchango wako moja kwa moja kwa kiongozi yeyote wa TASAO.

Naomba kuwasilisha.

Tunawasalimu pia wale wote mlio huko nyumbani Tanzania. Kila la kheri katika kujenga nchi yetu.
DEZIDERY KAJUNA
PRO