Mkurugenzi
wa habari na mawasiliano wa chama hicho Mh John Mnyika ameyasama hayo
alipokutana wa vyombo vya habari katika ofisi za makao makuu ya chama
hicho jijini Dar es salaam na kusema bado wahajajua ni hatua gani
watachukua mara baada ya kukamilika kwa mfululizo wa mikutano ya
sekretarieti ya chama inayoanza kesho chini ya katibu wa chama hicho Dk.
Wilbroad Slaa.
Kuhusu
uamuzi wa wabunge wa upinzani kutoka nje ya ukumbi wa bunge kwa lengo
la kutoshiriki kuchangia hoja muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba
mpya Mh Mnyika amesema hakubaliani na vipengele ambavyo vinakataka kutoa
fursa ya kuongeza idadi ya wawakilishi kuongezwa katika muswaada huo
ili kutoa haki ya ushiriki kwa makundi mengi zaidi katika jamii na
kupata katiba bora tofauti na ilivyo sasa, hivyo chama hicho kimesema
kitachukua hatua ya kurudi kwa wananchi ili kuwaeleza upungufu uliopo
katika muswaada huo ambao tayari wabunge wamekwisha upitisha na
kusubiriwa kuwa sheria baada ya rais kuusaini.
Wakati
huo huo Chama cha wananchi (CUF) kimelaani kitendo cha naibu spika Mh
Job Ndugai kuamuru askari wamtoe nje kiongozi wa kambi ya upinzani
bungeni Mh Freeman Mbowe kitendo walichokiita kuwa ni cha aibu na
hakikupaswa kufanya na kiongozi mkubwa kama huyo.
Hayo
yamesemwa na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho Mh Profesa Ibrahim
Lipumba wakati akizungumza makao makuu ya chama hicho jijini Dar es
salaam na kusema kuwa ni wazi kuwa kumekuwepo na upendeleo mkubwa
bungeni baina wabunge wa upinzani na wale wa chama tawala.
Aidha
kuhusu mchakato wa katiba mpya Profesa Lipumba amesema kuna njama za
wazi wazi ambazo zimekuwa zikifanywa ili katiba mpya iwe ya manufaa
kwa kundio moja na siyo kwa taifa zima.source: ITV-Daima