18 Septemba, 2013 - Saa 03:24 GMT
Rais wa Brazil Dilma Rousseff
amefutilia mbali mpango wake wa kusafiri nchini Marekani mwezi ujao
kutokana na madai kuwa Marekni ilikuwa inaipeleleza nchi hiyo.
Shirika la usalama wa kitaifa la Marekani (NSA)
limetuhumiwa kwa kunasa kisiri barua pepe na ujumbe mwingine kutoka kwa
Rais Rousseff, wasadizi wake na shirika la kitaifa la mafuta ,Petrobras.Rais wa Marekani Barack Obama aliahidi kuchunguza kisa hicho.
Ikulu ya White House iliwasiliana kwa njia ya simu na Rais Rousseff mnamo siku ya Jumatatu kujadili swala hilo.
Madai dhidi ya Marekani kuwafanyia udukuzi raia wa Brazil yalichapishwa kwa mara ya kwanza mwezi Julai na mwandishi wa habari wa jarida la Uingereza la Gurdian, nchini humo.
Greenwald alidai kuwa shirika la NSA liliweza kunasa taarifa zote za kuonyesha kuwa Bi Rousseff alikuwa kwenye mtandao.
SOOURCE: BBC SWAHILI