Kwa ufupi
Akitangaza matokeo ya uchagunzi huo, Chikawe
alisema Buriani amepata kura 316 na Mtanda ambaye pia ni Mbunge wa
Mchinga, amepata kura 1002.
Lindi. Wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM katika
Wilaya ya Lindi, wamemchagua kwa mara nyingine Saidi Mtanda kuwa mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM baada ya kumshinda mpinzani wake,
Shaibu Buriani kwa kura 600.
Uchaguzi huo ulifanyika juzi katika Kijiji cha
Kiwalala na kusimamiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Nachingwea, Abdalah Chikawe.
Akitangaza matokeo ya uchagunzi huo, Chikawe
alisema Buriani amepata kura 316 na Mtanda ambaye pia ni Mbunge wa
Mchinga, amepata kura 1002.
Mbunge wa Mtama, Benard Membe, aliwataka wajumbe kutumia hekima kuchagua kiongozi anayefaa.
Membe alisema CCM wilayani humo, inahitaji viongozi walio tayari kujitoa kwa ajili ya chama.
Uchaguzi huo umerudiwa baada ya CCM kupokea rufaa
na kutengua matokeo ya ule wa wali, uliokuwa umelalamikiwa na Buriani
(Mwanja Ibadi)
source: Mwananchi
source: Mwananchi