Mbunge wa Mfenesini (CCM), Suleiman Nassib Omar akiweka saini baada ya 
Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangala (kushoto) kuanza kukusanya saini 
za wabunge kwenye ukumbi wa bunge jana akitafuta kuungwa mkono katika 
hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda.PICHA NA EDWIN
 MJWAHUZI 
            
    Na Neville Meena na Sharon Sauwa, Mwananchi
Posted Ijumaa,Novemba1 2013 saa 24:0 AM
Posted Ijumaa,Novemba1 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Spika anasema mbunge yeyote ana haki kwa mujibu wa 
Kanuni za Bunge kuwasilisha hoja ya kumng’oa, lakini yeye hatetereki kwa
 sababu hajavunja kanuni yoyote ya Bunge.
Dodoma: Spika wa Bunge, Anne 
Makinda amesema hatishwi na mchakato wa kumng’oa katika nafasi yake 
ambao umeanzishwa na Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangalla kutokana na
 tuhuma za kukiuka kanuni za Bunge.
Kadhalika Spika Makinda amepuuza hoja za Dk 
Kigwangalla akisema kuwa yeye hajavunja kanuni yoyote, lakini akaweka 
bayana kuwa mbunge huyo wa Nzega ana haki kwa mujibu wa Kanuni za Bunge 
kuendelea na kile anachokifanya.
“Kanuni si zinamruhusu, utaratibu upo kwenye 
kanuni za Bunge kwa hiyo aendelee na mchakato lakini mimi ninachosema 
sitetereki maana hakuna kanuni yoyote ambayo nimeivunja,” alisema 
Makinda katika mahojiano maalumu na Mwananchi ofisini kwake jana.
Wakati Spika akitoa kauli hiyo, jana, Dk 
Kigwangalla alianza harakati zake za kukusanya saini za wabunge, 
akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani naye kwa madai 
kwamba amekuwa akikiuka kanuni.
Miongoni mwa madai ya Dk Kigwangalla ni hatua ya 
Makinda kufanya uteuzi wa Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge 
kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, tofauti na kanuni 
zinazotaja wenyeviti kuchaguliwa na wajumbe wa kamati.
Hoja nyingine ni kamati hiyo ya bajeti kulipwa 
posho ya Sh430,000 wakati wajumbe wa kamati nyingine wamekuwa wakipewa 
Sh130,000 pamoja na kumteua Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba 
kuingia katika kamati hiyo ya bajeti wakati mbunge huyo ni Mwenyekiti wa
 Kamati ya Miundombinu.
Jana Dk Kigwangalla aliwasilisha hoja yake kwa 
Katibu wa Bunge na kuongeza madai mapya yakiwamo ya kuagiza kwa mabavu 
majedwali ya mabadiliko ya sheria kwenda kwenye kamati ya bajeti, 
kuvunja masharti ya kanuni ya 48 inayotoa maelekezo ya namna ya 
kuwasilisha na kujadili jambo la dharura na kutumia madaraka yake vibaya
 kwa kuvunja masharti ya Sheria ya The National Assembly 
(Administration) Act (Cap.115) ya mwaka 2008.
Makinda akijibu hoja hizo jana alisema alifanya 
uteuzi wa Chenge kuongoza Kamati ya Bajeti kwa sababu kamati hiyo ni 
mpya na haikuwapo katika kamati za awali, hivyo ni wazo ambalo 
lilitokana na mawazo ya Bunge la sasa.
“Tulikuwa tunafikiria jinsi Bunge linavyoweza 
kuisadia Serikali ipate vyanzo vipya vya mapato. Kwa hiyo tumehitimisha 
wazo hili kwa kuamua kuwa na Kamati ya Bajeti. Kamati hii haikuwapo na 
wala utaratibu wake wa kikanuni haukuwapo. Niliamua na kanuni zinanipa 
uwezo huo kwamba niteue mtu ambaye ninaamini anaweza kuisimamia katika 
hatua za mwanzo ili tuone uzoefu utatufikisha wapi,” alisema Makinda na 
kuongeza:
“Kamati hii hata Serikali ilikuwa haikubaliani na 
sisi, lakini katika muda mfupi wa utendaji wake umefanya kazi kubwa na 
kama tusingekuwa na Mzee Chenge ambaye ni mzoefu na anafahamu vizuri 
utendaji wa Serikali basi tungeshindwa na mimi siko tayari kuanzisha 
kitu halafu nikashindwa”.
Kuhusu posho, Spika aliungana na kauli ya Katibu 
wa Bunge, Dk Thomas Kashililah kwamba si wakati wote Kamati ya Bajeti 
imekuwa ikipewa malipo zaidi, bali ni pale tu wanapofanya kazi nje ya 
siku na saa za kazi tena kwa kibali chake.
“Lazima walete maombi na waeleze kwa nini 
wanapaswa kufanya kazi kwa muda wa ziada au siku za mapumziko na mimi 
nikisharidhia basi wanalipwa mara mbili ya viwango vya kawaida na hiyo 
ni kwa mujibu wa taratibu na Kanuni zetu,” alisema.
SOURCE: MWANANCHI
Kadhalika alizungumzia suala la wabunge wengine kuteuliwa 
kuingia kwenye kamati ambazo si zao ambapo alisema, suala hilo pia ni la
 kawaida kwani hata katika mjadala unaoendelea wa Kamati ya Katiba, 
Sheria na Utawala ameongeza wajumbe wa ziada.
“Ninafanya hivyo kupanua wigo wa mjadala na mara 
nyingi kwa mfano kwenye kamati yetu ya Katiba nimeongeza wabunge wenye 
uelewa wa masuala ya sheria ili watusadie kufanya uchambuzi, maana 
unaweza kukuta kwenye kamati, watu wenye utaalamu kuhusu suala husika ni
 wachache. Kwa hiyo siyo kosa kwa mujibu wa Kanuni zetu,” alisema 
Makinda.
Ukusanyaji saini
Kwa upande wake Dk. Kingwangalla jana alikuwa 
akiendelea na ukusanyaji wa saini za wabunge huku akisema kuwa 
amewasilisha kwa Katibu wa Bunge kusudio la kupeleka bungeni hoja yake.
Ukusanyaji wa saini ulifanywa kwa kupitia fomu 
maalumu na kutoa taarifa kwamba wabunge wa CUF na NCCR-Mageuzi, wote 
wameshasaini katika fomu hizo.
Akizungumza jana katika viwanja vya Bunge, Dk 
Kigwangallah, alisema wabunge wa Chadema, walimweleza kuwa watafanya 
hivyo baada ya kukutana katika kikao cha pamoja.
Hata hivyo Kiongozi wa Upinzani Bungeni ambaye pia
 ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alikiri kusikia taarifa hizo 
lakini akasema walikuwa bado hawajaketi kama kambi ili kuwa na msimamo 
wa pamoja kuhusu suala hilo.
Jana asubuhi wakati wa kipindi cha maswali na 
majibu, Dk. Kingwangalla alionekana akipita katika baadhi ya meza za 
wabunge akiwashawishi kusaini fomu za kumuunga mkono.
Hadi jana mchana wabunge wa CCM, na CUF wapatao 30 tayari walikuwa wamesaini fomu hizo, wakimuunga mkono mbunge huyo.
Alipoulizwa ulazima wa kukusanya saini za wabunge 
wakati kanuni hazimtaki kufanya hivyo alisema, hilo linamwezesha kujua 
nguvu aliyonayo katika kumuunga mkono kuhusiana na suala hilo.
Hoja zake
endelea kusoma habari hii:  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-Siogopi-hoja-ya-kung-olewa-/-/1597296/2055480/-/item/2/-/xdq4wiz/-/index.htmlSOURCE: MWANANCHI