Saturday, 7 September 2013

Baadhi ya maoni ya Watanzania waliyo toa kwenye ukurasa wa gazeti maarufu Mwananchi juu ya mkutano wa Kikwete na Kagame kule Uganda


  • Avatarkasome
    Kuaminiana ni jambo la msingi sana katika mashirikiano yoyote. Mimi sijui kama kuna waTanzania wengi sasa wanaoweza kusema kwamba tunawaamini hawa washirika wenzetu wanaoamua kufanya mambo yao bila ya kutushirikisha. Kama hizi zilikuwa ni mbinu za kutulainisha ili tuwakubalie kila wanalotaka; matumaini yangu ni kwamba viongozi wetu hawatateteleka kabisa. Acha wajirushe wanavyotaka, sisi tufuate tu programu ileile tuliyojiwekea kama bado tunataka kuendelea kuwa katika umoja huu. Hawa hawana njia ya kuiepuka Tanzania inayoinukia - watakuja tu kutupigia magoti watake wasitake. Lakini tusikubali watuvuruge.

  • simon mukama
    museveni aendelee na juhudi zake kama kawaida na mimi kimsingi nadhani kila kiongozi katika EAC,anao uhuru wa kutoa mawazo yake na yanaweza kukubaliwa ama kukataliwa na yeyote,so nampongeza Kagame kama ameona kuukataa ushauri wa Kikwete una tija yoyote kwake na nchi yake na pia sio lazima ukakubali ushauri wa kila mtu coz hata Nyerere aliwahi kusema wazizwazi kuwa hampendi Idd Amin na huo ndo ulikuwa msimamo na mtizamo wake,however Kikwete anaweza kuendelea kutoa ushauri kwa watu but lazima aangalie anautolea wapi na mazingira gani na pia ni ushauri wa aina gani anutoa.

  • Steven Mamba
    "Kwa mujibu wa taarifa Rais Museveni ameitisha mkutano huo hasa kuzungumzia hatua ya Umoja wa Mataifa kupambana na Kundi la Waasi wa M23." Kama kuna watu hadi sasa hawajui M23 ni waasi kutoka Rwanda basi wote tuna matatizo ya akili
  • Mboya
    Ni jambo la heri. ila inaonekana kuwa Kagame na Museveni lao moja hata kwenye kuhama bandari ya Dar na kusaini mkataba na Kenya walikua pamoja. Ni vyema waache unafki waelewane!!

  • Analyst7
    Sasa simwamini tena Museveni. Naona kama anakwenda kwa mama Maria Nyerere na kumwambia wewe ni mama yangu kabisa nitakusikiliza ushauri wako siku zote. Akitoka hapo anaenda kwa JK na kumwambia sisi sote ni ndugu na protegees wa Nyerere, na mimi nimekulia Tanzania hivyo hapa ni nyumbani. Akitoka hapo anaenda kwa Kagame anamwambia JK asitubabishe kabisa, sisi tuendelee na mipango yetu wala hatumuhitaji JK na Tanzania yake kwa sababu EAC inawezekana bila JK na Tanzania.

  • Minja, Joseph
    EAC ni mali ya wananchi wa nchi husika na ni tofauti kabisa na EAC ya zamani. Hivyo nchi na nchi zinaweza kutofautiana sana na viongozi wake wasipende hata kuonana na EAC ikawa bado ipo. Juhudi za Mhe, Museveni hazina budi kupongezwa kwani zikizaa matunda mazuri uhasama utakwisha. Pamoja na hayo, kuna ubaya gani Mhe. Museveni akikutanisha M23 na Mhe. Kagame kwanza halafu na wakuu wenzake wa maziwa makuu (ICGLR) kuwaelezea yanayojiri kati yao na nini kifanyike?


    Source : Mwananchi