Saturday, 7 September 2013

‘Mgomo hasara Tazara’


Na Sharon Sauwa, Mwanachi

Posted  Septemba7  2013  saa 11:55 AM
Kwa ufupi
Serikali imewataka tena wafanyakazi hao kurejea kazini bila kukosa ifikapo Septemba 9 mwaka huu na kufanya kazi kwa bidii ili kufidia hasara iliyotokana na mgomo huo.


Dodoma. Mgomo wa wafanyakazi wa Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), uliodumu wa kwa wiki mbili, umesababisha hasara ya zaidi ya Dola 14 milioni za Marekani.
Serikali imewataka tena wafanyakazi hao kurejea kazini bila kukosa ifikapo Septemba 9 mwaka huu na kufanya kazi kwa bidii ili kufidia hasara iliyotokana na mgomo huo.
Hayo yalisemwa bungeni jana na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, alipokuwa akiwasilisha kauli ya mawaziri kuhusu mgomo wa wafanyakazi wa Tazara.
Kauli hiyo ni utekelezaji wa agizo la Naibu Spika, Job Ndugai, alipokuwa akijibu mwongozo wa Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Kiwanga (Chadema) Jumatatu wiki hii.
Dk Mwakyembe alisema mgomo huo umesababisha treni 13 zenye mabehewa 252 ya mzigo kukwama njiani.
“Zaidi ya abiria 24,000 wenye tiketi wakimo watalii walikosa huduma ya usafiri wa treni.
“Wameshalipwa mishahara ya Mei mwaka huu na kuwa ifikapo Jumatatu (Septemba 9 mwaka huu) watalipwa mishahara yao ya Juni, Julai na Agosti.
Alisema Serikali mbili zimeagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Tazara kukutana mapema iwezekanavyo kwa ajili ya maandalizi ya kikao cha Baraza la Mawaziri ndani ya Septemba mwaka huu .
Lengo la kikao hicho ni kutafakari ili hali iliyojitokeza na kuchukua hatua mara moja ili hali hiyo isijitokeze tena.
Mgomo huo ulianza Septemba 2 mwaka huu, uliitishwa na Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Trawu), kudai malimbikizo ya mishahara ya miezi minne.

source: Mwananchi