Kwa ufupi
Tafiti nyingi zinaonyesha wanawake wa asili ya Kiafrika wanapata zaidi tatizo hili kuliko wazungu.
Hujulikana kwa lugha ya kigeni kama uterine myoma, fibroid. Ni wazi kwamba tatizo hili linawakumba zaidi wanawake.
Huwapata kwa asilimia tano wanawake wenye umri 
kati ya miaka 20 hadi 30, asilimia karibu 20 kwa wenye umri kati ya 
miaka 30 hadi 40, na zaidi ya asilimia 40 kwa wale wenye umri zaidi ya 
miaka 40.
Hii inamaanisha kwamba kadiri umri unavyokuwa 
umkubwa mwanamke ana nafasi kubwa ya kupata ugonjwa huu, pia nitatizo 
kubwa katika jamii kwa sasa, ikizingatiwa kwa ukubwa kwamba inahusu 
mfuko wa uzazi.
Pia utaona kwamba huwakumba zaidi kina mama ambao wako katika umri wa kuweza kuzaa (reproductive age).
Uvimbe huwa wa saizi mbalimbali, huanza kuwa 
mdogo, na baadaye kuwa mkubwa sana na mwanamke kuonekana kama anatumbo 
la uzazi (mjamzito).
Uvimbe huu unaweza kuwa mmoja lakini wakati hutokea uvimbe zaidi ya mmojaamboa hutanda katika mfuko wa uzazi.
Tafiti nyingi zinaonyesha wanawake wa asili ya Kiafrika wanapata zaidi tatizo hili kuliko wazungu.
Huwapata pia zaidi wanawake ambao hawajazaa 
kabisa, kubahatika kutunga mimba na kuzaa (Nulliparity), wanawake 
wanene, au kuwepo kwa ndugu wa karibu aliyepatwa na ugonjwa huu mfano 
mama na dada.
Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kutokwa damu 
nyingi sana kwa muda mrefu wakati wa hedhi ikiambatana na mabonge 
mabonge isivyo kawaida.
Dalili nyingine ni kupata maumvi ya kiuno, ugonjwa
 kubana viungo vingine vya mwili (pressure symptoms) hivyo kupumua kwa 
shida au kukojoa mara kwa mara au kushindwa kupata choo kikubwa kawaida.
 Nyingine ni pamoja na kutokutunga mimba, au mimba kuharibika na kutoka.
Uchunguzi
Nirahisi kwa mtaalamu kugundua ugonjwa huu au 
uvimbe katika mfuko wauzazi kwa kumkagua, au kumpima mgojwa (bimanual 
examination).
Itaendelea wiki ijayo...
source: Mwananchi
Itaendelea wiki ijayo...
source: Mwananchi
