Posted 
    Jumapili,Septemba1 
2013 
saa
14:15 PM
            
Kwa ufupi
Ilichukua miaka minne kwa kundi hilo kufikishwa
 mahakamani. Lakini kwa Wachina muda huo haukuwa tatizo kwani kiu yao 
ilikuwa ni kujua ukweli katika hilo.
 
        
  
   
  
            
Beijing (CNN) – Kesi ya Bo Xilai, mwanamume 
ambaye nyota yake ilikuwa iking’aa na kutajwa kuwa kati ya watu 25 wenye
 nguvu nchini China sasa anaelekea ukingoni.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba hata kama 
atashinda, lakini heshima aliyokuwa nayo, ambayo ingemwezesha kushika 
madaraka haitakuwepo tena, hivyo ndoto zake kisiasa zitakuwa zimekoma 
kwa kuwa nchini humo hakuna sheria itakayomruhusu kuwania uongozi na 
pengine ndiyo hasa lilikuwa lengo la mlolongo mzima wa kesi aliyonayo.
Huku kesi hiyo ikitawaliwa na visa vya mapenzi, 
ulaghai na ushahidi wa video, imekuwa na mvuto wa kipekee na kubatizwa 
jina la ‘Kesi ya Muongo’.
Ingawa inatajwa kuendeshwa kwa uhuru na haki, 
picha chache na video zilizohaririwa zimekuwa zikirushwa mtandaoni na 
mahakama inayosikiliza kesi hiyo.
Watu wachache waliopata bahati ya kuhudhuria kesi 
ya Bo, wanasema kuwa kama kila kinachoendelea katika mahakama hiyo 
kingewekwa wazi, angekuwa na nafasi kubwa ya kushinda, lakini imekuwa 
ndivyo sivyo.
Bo anakumbusha kesi kama hiyo iliyowahi kutokea 
katika miaka ya 80 iliyojulikana kama ‘Gang of Four’ iliyowahusisha 
vigogo wa nchi hiyo wanne.
Kundi hilo la watukutu likiongozwa na Jiang Zedong
 aliyekuwa mjane wa Mao na washirika wake watatu ilivuta hisia za watu 
duniani kote kutokana na namna ilivyoendeshwa.
Qing ambaye alijipatia umaarufu na kupata wadhifa 
wa juu katika Chama cha Kikomunisti cha China kabla ya kuangushwa 
akituhumiwa kutaka kufanya mapinduzi.
Mwezi mmoja baada ya mumewe kuuawa mwaka 1976, 
kundi hilo la watu wanne na washirika wao wengine walikamatwa kwa makosa
 ya uhaini, pia kuhusishwa kutaka kumuua Mao.
Ilichukua miaka minne kwa kundi hilo kufikishwa 
mahakamani. Lakini kwa Wachina muda huo haukuwa tatizo kwani kiu yao 
ilikuwa ni kujua ukweli katika hilo.
Zaidi ya watu 600, wengi wakiwa viongozi wa 
Serikali, wawakilishi wa jamii , waandishi wa kuaminika na ndugu wa 
watuhumiwa, walikuwa wakihudhuria kesi hiyo.
Kesi hiyo ilikuwa habari kubwa duniani kote, 
iliripotiwa na nchi mbalimbali kwa mapana. Wakati ule China ndiyo kwanza
 ilikuwa imetoka katika utawala wa kidikteta wa Mao.
 
Aidha, kesi hiyo ilidumu kwa miezi miwili. Kwa 
waandishi wa nje walitegemea habari kutoka kwa waandishi walioaminiwa na
 Serikali.
Miongoni mwa mambo yaliyovutia katika kesi hiyo ni
 pale, Jiang Qing alipojitetea kuwa kila alichokifanya ilikuwa ni kutii 
matakwa ya Mao, akijifanaisha na mbwa.
Jiang alipiga kelele akisema: “Nilifanya yote kwa 
ajili ya Mao, mimi nilikuwa mbwa wake niliyemng’ata kila aliye mbele 
yangu kwa maelekezo ya bosi wangu.”
Katika hotuba yake ya mwisho, ambayo ilichukua 
muda wa saa mbili, mwanamke huyo aliyekuwa na umri wa miaka 66 alisema 
yuko tayari kufa kwa sababu kila alichokifanya ilikuwa ni kwa ajili ya 
kumuenzi mume wake.
Mwanzoni mwa mwaka 1981, Madame Mao, kama 
alivyokuwa akijulikana alihukumiwa kifo, lakini miaka mkichache baadaye 
alijiua wakati akiwa katika kifungo cha nyumbani.
Biashara kama kawaida
Bado kuna mambo hayajabadilika, hata baada ya kubadilisha mfumo wa mahakama katika miaka ya karibuni.
Mfano mwaka 1981, mahakama iliibatiza jina la kesi
 ya Biao na wenzake kwa kuuita, “ Kesi ya Lin Biao na Jiang Quing kundi 
lililotaka kufanya mapinduzi.” Kichwa hicho cha habari kinamhukumu 
mtuhumiwa moja kwa moja, hata kabla ya kesi kuanza kusikilizwa.
Miongo mitatu baadaye, hakuna kesi kubwa 
iliyoashiria kuwa mtuhumiwa anaweza kushinda. Unaposikia kesi ikianza 
kuunguruma, tayari inakuwa imeshatoa hukumu. Katika kesi ya Bo, 
wachambuzi wa mambo ya siasa wanasema uongozi mpya wa Rais Xi Jinping 
unataka kujihakikishia kuwa unashinda bila kubaki na ‘damu mikononi’.
Kwa kuwa Bo anagomea kukiri kile ambacho Serikali 
inataka afanye, suala hilo zito ndilo linaloiweka njia panda kesi hiyo 
katika kutoa hukumu.
Imetafafsiriwa na Julieth Kulangwa kutoka cnn.com
source: Mwananchi