Rais wa Rwanda Paul Kagame, akizungumza na vyombo vya habari hivi 
karibuni, .Marekani imeitaka Serikali ya Rwanda kutoa ushirikiano 
utakaosaidia kuacha  mapigano  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.PICHA | 
MAKTABA 
            
Posted Jumanne,Oktoba8 2013 saa 13:28 PM
Kwa ufupi
Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa 
Samantha Power alisema kuwa, Rwanda ikiwa ni nchi jirani na Kongo 
inapaswa kuwa na nafasi ya moja kwa moja katika mchakato wa kuleta amani
 na utulivu nchini Kongo.
Washington.Marekani imeitaka Serikali ya Rwanda 
kutoa ushirikiano utakaosaidia kuacha  mapigano  Jamhuri ya Kidemokrasia
 ya Kongo.
Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa 
Samantha Power alisema kuwa, Rwanda ikiwa ni nchi jirani na Kongo 
inapaswa kuwa na nafasi ya moja kwa moja katika mchakato wa kuleta amani
 na utulivu nchini Kongo.
Power alisisitiza kwamba nchi zote za eneo la 
Maziwa Makuu ya Afrika zinapaswa kufanya juhudi maradufu za kuwatokomeza
 waasi walioko mashariki mwa nchi hiyo.
Juzi  ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa 
Mataifa uliyataka makundi ya waasi mashariki mwa Kongo kuacha kuendeleza
 machafuko katika eneo hilo.
Serikali ya Jamhuri ya Kongo imeshakaa na 
wapiganaji wa kundi la M23 mara kadhaa lakini mpaka sasa bado hakuna 
makaubaliano kamili baina yao.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI
