05: Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, Agrey Mwanri akiwaonyesha wananchi ufa za ukuta wa choo wa soko
la Makuyuni Wilayani Korogwe Mkoani Tanga, ambapo zaidi ya Sh500
milioni zimeshatumika katika ujenzi wa soko hilo na bado halijakamilika
na baadhi ya kuta za majengo ziko hatarini kuanguka. PICHA | SALIM
MOHAMMED
Na Salim Mohammed, Mwananchi
Posted Ijumaa,Oktoba4 2013 saa 19:17 PM
Posted Ijumaa,Oktoba4 2013 saa 19:17 PM
Kwa ufupi
- Ujenzi wa soko la Makuyuni ambalo lilianza mwaka
2008 na kutarajiwa kukamilika 2009, limeshindwa kukabidhiwa kwa
halmashauri kwa kile kinachodaiwa kufanyika kwa ubadhirifu wa pesa za
Serikali.
Korogwe. Naibu Waziri, Ofisi
ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Agrey
Mwanri amemwagiza Katibu Tawala pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya
Korogwe kuunda timu ya uchunguzi wa ujenzi wa Soko la Makuyuni unao
daiwa kugharimu zaidi ya Sh500 milioni huku ujenzi huo ukishindwa
kukamilika.
Ujenzi wa soko la Makuyuni ambalo lilianza mwaka
2008 na kutarajiwa kukamilika 2009, limeshindwa kukabidhiwa kwa
halmashauri kwa kile kinachodaiwa kufanyika kwa ubadhirifu wa pesa za
Serikali.
Akizungumza mara baada ya kulikagua soko hilo,
Mwanri alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Korogwe, Lucas
Mweri kuhakikisha ndani ya siku 30 soko hilo linafanya kazi ikiwa ni
pamoja na kukamilisha ujenzi wake.
"Ndugu wananchi hapa kuna tatizo na siamini kuwa
Sh500 milioni zimeshindwa kujenga kasoko haka na kuomba katibu tawala
kuunda timu ya uchunguzi juu ya hili soko ...mimi siamini,” alisema
Mwanri.
Mwanri alisema hatokuwa tayari kuona pesa za
Serikali na nguvu za wananchi zikifujwa na wajanja na kusema kuwa mtu
yeyote anayefanya ufisadi atachukuliwa hatua na kurejesha pesa
alizochukua.
Alisema soko hilo ambalo hata kukamilika kwake ni
utata limeanza kukatika kuta zake pamoja na vyoo kubomoka na hivyo
kuitaka kamati ya ujenzi kuwaeleza wananchi mamilioni ya pesa
zilivyotumika.
Akisoma taarifa ya ujenzi huo, Mhandisi wa soko
hilo, Lucas Mweri, alisema ili kuweza kukamilika kwa ujenzi huo
zinahitajika Sh28 milioni zaidi zikiwa ni pamoja na kuweka vizimba vya
biashara.
Alisema soko hilo limeshindwa kukamilika baada ya
kuishiwa pesa na hivyo kuitaka halmashauri kuidhinisha kiwango hicho ili
kuweza kukamilisha ujenzi huo na kuanza wananchi kulitumia.
Alisema soko hilo ambalo litatumika kuuzia
stakabadhi ghalani pamoja na wananchi kuuza na kununua bidhaa, litakuwa
ni mkombozi wa wakulima wa mahindi na mbogamboga wakiwamo wa makabichi
na nyanya.
SOURCE: MWANACHI
SOURCE: MWANACHI