Saturday, 7 September 2013

Mbunge Mkosamali ‘aichokonoa’ Serikali


Na Habel Chidawali, Mwananchi

Posted  Septemba7  2013  saa 11:46 AM
Kwa ufupi
Mkosamali alitoa kauli hiyo jana kupitia swali lake nyongeza.
“Je Serikali haioni kuwa huo ni ubaguzi na ndio maana mzee Mrema anajikomba huko,” alisema Mkosamali.


Dodoma. Mbunge (Muhambwe-NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali jana aliichokonoa Serikali kwa kuhoji sababu za kutomlipa mafao yake Augustino Mrema ambaye amekuwa akijikomba kwa muda mrefu.
Mkosamali alitoa kauli hiyo jana kupitia swali lake nyongeza.
“Je Serikali haioni kuwa huo ni ubaguzi na ndio maana mzee Mrema anajikomba huko,” alisema Mkosamali.
Kauli hiyo ilitafsiriwa kuwa ni sehemu ya kumshushia vijembe Mrema ambaye juzi aligoma kujiunga na wabunge wenzake wa upinzani katika kuupinga muswaada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013.
Mrema ambaye ni Mbunge wa Vunjo kupitia tiketi ya TLP, amekuwa na ugomvi na Serikali kuhusu kutolipwa mafao yake ya kuitumikia nchi katika nafasi ya Naibu Waziri Mkuu katika kipindi cha utawala wa Serikali ya awamu ya pili.

source: Mwananchi