Na Habel Chidawali, Mwananchi
Posted Septemba7 2013 saa 11:46 AM
Posted Septemba7 2013 saa 11:46 AM
Kwa ufupi
Dodoma. Mbunge (Muhambwe-NCCR-Mageuzi), Felix
Mkosamali jana aliichokonoa Serikali kwa kuhoji sababu za kutomlipa
mafao yake Augustino Mrema ambaye amekuwa akijikomba kwa muda mrefu.
Mkosamali alitoa kauli hiyo jana kupitia swali lake nyongeza.
“Je Serikali haioni kuwa huo ni ubaguzi na ndio maana mzee Mrema anajikomba huko,” alisema Mkosamali.
Kauli hiyo ilitafsiriwa kuwa ni sehemu ya
kumshushia vijembe Mrema ambaye juzi aligoma kujiunga na wabunge wenzake
wa upinzani katika kuupinga muswaada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba
wa mwaka 2013.
Mrema ambaye ni Mbunge wa Vunjo kupitia tiketi ya
TLP, amekuwa na ugomvi na Serikali kuhusu kutolipwa mafao yake ya
kuitumikia nchi katika nafasi ya Naibu Waziri Mkuu katika kipindi cha
utawala wa Serikali ya awamu ya pili.
source: Mwananchi
source: Mwananchi