Na Frederick Katulanda, Mwananchi
Posted Septemba7 2013 saa 11:41 AM
Posted Septemba7 2013 saa 11:41 AM
Kwa ufupi
Mwanza. Mamlaka ya Usafirishaji ya Udhibiti 
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra),imeagiza wasafirishaji 
wanaotumia vyombo vya majini kanda ya ziwa kupitia Bandari zote Ziwa 
Victoria kusafirisha abiria mwenye kitambulisho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,Meneja wa 
Sumatra Kanda ya Ziwa, Mhandisi Japhet Ole Loisuimaye alisema, utaratibu
 huo umelenga kuhakikisha kuna kuwa taarifa za kina kwa kila abiria 
anayesafiri na meli ama boti ndani ya Ziwa Victoria.
Alisema utaratibu huo utaanza kutumika Septemba 9,
 mwaka huu na kubainisha kwamba kila abiria atapaswa kuwa na moja kati 
ya kitambulisho kifuatacho, Kitambulisho cha Uraia, cha Ukaazi, Paspoti,
 cha Kupigia Kura, Kazi, Leseni ya Udereva ama kwa wale wasiokuwa na 
hivyo vyote basi wawe na barua toka Serikali za Mitaa yenye picha.
“Agizo hili limetolewa na Serikali kwa lengo la 
kuhakikisha kunakuwa na kumbukumbu sahihi za abiria (passenger manifest)
 wote wanaosafiri na meli ama boti kwa umbali usiozidi maili za majini 
(noutcal miles) 20 kati ya bandari, hivyo agizo hili halitawahusu abiria
 wanaosafiri na vivuko,” alifafanua. Alisema agizo hilo linapaswa 
kufuatwa na wasafirishaji wote kwa vile ni utekelezaji wa Kanuni za 
Kuhakiki na kusajili abiria kama zilivyoainishwa.
source: Mwananchi
source: Mwananchi