Rais Paul Kagame
Posted Jumatatu,Oktoba7 2013 saa 16:47 PM
Kwa ufupi
Bunge hilo linatarajiwa kupitia ripoti mbalimbali za kamati za kisekta na kuzithibitisha.
Kigali. Spika mpya wa Bunge la
Rwanda, Donatille Mukabalisa ameanza kuzimamia vikao vya Bunge baada ya
kuapishwa rasmi Ijumaa iliyopita.
Katika vikao hivyo vilivyoanza leo Jumatatu, moja
ya majukumu muhimu kwa wabunge hao ni kupitia na kuthibitisha agenda
muhimu za kusimamiwa na Bunge hilo.
Bunge hilo lilichaguliwa kupitia uchaguzi mkuu wa
Bunge uliofanyika Agosti mwaka huu na kutoa wingi wa viti kwa chama
tawala cha RPF chini ya Rais Paul Kagame.
Wabunge hao wamepewa jukumu la kupitia na
kuharakisha miswada muhimu iliyokuwa imewekwa kiporo na masuala muhimu
yanayotakiwa kupewa kipaumbele ili kuharakishwa na Serikali.
Mkuu wa Mawasiliano wa Bunge hilo, Augustin
Habimana amesema kwamba yapo mambo mengi yanayotarajiwa kupitiwa na
Bunge hilo ikiwemo kupanga ratiba ya kujadiliwa kwa miswada hiyo na
kupitishwa.
Pia Bunge hilo linatarajiwa kupitia ripoti mbalimbali za kamati za kisekta na kuzithibitisha.
Bunge linao wajibu wa kupokea, kujadili na kutoa
mapendekezo yatakayosaidia kupitishwa kwa miswada 13 iliyoshindwa
kupitishwa kwenye Bunge lililopita.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI