Kamanda wa polisi mkoani Geita,Leonard Paulo
Na Salum Maige, Mwananchi
Posted Jumatatu,Oktoba7 2013 saa 14:33 PM
Posted Jumatatu,Oktoba7 2013 saa 14:33 PM
Kwa ufupi
Marehemu huyo ametajwa kuwa ni, Maua Ikoti(60) mkazi wa Kasang'hwa, wilayani Geita .
Mauaji hayo yamekuja huku takwimu zikionyesha kuwa vikongwe watatu, wameuawa na kikundi hicho katika kipindi cha wiki nne zilizopita.
Mauaji hayo yamekuja huku takwimu zikionyesha kuwa vikongwe watatu, wameuawa na kikundi hicho katika kipindi cha wiki nne zilizopita.
Geita. Mauaji ya kikatili
yanayodaiwa kufanywa na Kikundi cha Chinjachinja dhidi ya vikongwe,
yamezidi kuutikisa Mkoa wa Geita baada ya kikongwe mwingine, kuuawa kwa
kukatwa kwa mapanga akiwa nyumbani kwake.
Marehemu huyo ametajwa kuwa ni, Maua Ikoti(60) mkazi wa Kasang'hwa, wilayani Geita .
Mauaji hayo yamekuja huku takwimu zikionyesha
kuwa vikongwe watatu, wameuawa na kikundi hicho katika kipindi cha wiki
nne zilizopita.
Baadhi ya watu wanahusisha maujai hayo na imani za kishirikina.
Tukio la mauaji hayo lilitokea saa 6 usiku wa
kuamkia juzi baada ya wauaji kuvamia familia hiyo na kisha kuingia
ndani ya chumba alimokuwa amekala kikongwe huyo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kasang'hwa,
Maganiko Ndiomali, alisema wauaji walimkata kwa mapanga kikongwe huyo
kichwani,mikono na kwenye matiti.
Alisema pamoja na mayowe yaliyopigwa na watoto wa
marehemu ili kuomba msaada, juhudi za wananchi kuwasaka wauaji hazikuzaa
matunda.
Kuna madai kuwa kikundi kinachohusishwa na mauaji
hayo kimekuwa kikodiwa na baadhi ya watu ili kulipiza kisasi baada ya
kufiwa na ndugu zao wakiamini kwamba wamerogwa.
Kikundi hicho kinadaiwa kuhusika na mauaji ya
kikatili dhidi ya Mondesta Nchambi (53) mkazi wa kitongoji cha Isabilo
wilayani Chato kwa kumchinja mithili ya kuku.
Kamanda wa polisi mkoani Geita,Leonard Paulo
alithibitisha kuwepo kwa matukio hayo lakini alisema hadi sasa hakuna
mtu au watu waliokamatwa wakihusishwa na mauaji hayo.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI