Na Habel Chidawali na Sharon Sauwa,Mwananchi
Posted Ijumaa,Novemba1 2013 saa 24:0 AM
Posted Ijumaa,Novemba1 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira alisema shida waliyonayo wananchi
wa Isimani ni sawa na maeneo mengine nchini .
Dodoma. Spika wa Bunge, Anne
Makinda jana aliingilia kati mvutano baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi baada ya kubanwa na
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Chiku Abwao.
Hali hiyo ilijitokeza pale Lukuvi alipolazimika
kutumia nafasi yake ya uwaziri kujibu swali la nyongeza lililoulizwa na
Abwao kuhusu mpango wa serikali wa kufikisha maji Isimani. “Mheshimiwa
Waziri, Jimbo la Isimani wananchi wake wana matatizo makubwa ya
upatikanaji wa maji na wamekuwa na maisha magumu,hivyo wanahitaji msaada
huo, je Serikali inatoa kauli gani kuhusu kuwasaidia wananchi hao,”
aliuliza Abwao.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira alisema shida waliyonayo wananchi
wa Isimani ni sawa na maeneo mengine nchini .
Baada ya majibu hayo, Lukuvi alilazimika kusimama
ghafla na kuwasha kipaza sauti,ili kusawazisha jibu la swali hilo ambalo
lililenga moja kwa moja katika jimbo lake,Baadhi ya wabunge walianza
kupiga kelele za kumtaka Lukuvi asizungumze kwa kuwa swali lilimlenga
moja kwa moja.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI