Na Florence Majani, Mwananchi
Posted Ijumaa,Novemba1 2013 saa 24:0 AM
Posted Ijumaa,Novemba1 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Ripoti hiyo ya Uhalifu wa Kiuchumi ya mwaka 2013
iliyotolewa na Kampuni ya Uchunguzi wa Huduma ya Delloite imebaini kuwa
watendaji wa ngazi za juu wanahusika zaidi na uhalifu huo ukilinganisha
na watendaji wa ngazi za chini.
Dar es Salaam.Taasisi za Fedha
nchini zimepoteza kiasi cha Sh34.4 bilioni kuanzia kipindi cha Oktoba
mwaka jana hadi Oktoba mwaka huu kutokana na wizi wa fedha katika
taasisi hizo,ripoti mpya imebainisha.
Utafiti huo uliofanyika katika nchi za
Kenya,Tanzania na Uganda umebainisha kuwa,Taasisi za Fedha za Afrika
Mashariki zimepoteza zaidi ya Sh471 bilioni sawa na (USD 30 milioni) kwa
mwaka.
Hata hivyo benki hizo ziliweka wazi upotevu wa
Sh126.9 bilioni tu ambao ni robo ya upotevu huo wa zaidi ya Sh471
bilioni kwa kile kinachodaiwa kuhofia kupoteza wateja.
“Taasisi za fedha zinapoteza fedha nyingi kutokana
na teknolojia na watendaji wa ngazi za juu kuhusika kwa kiwango kikubwa
lakini hazitaki kukiri kwa sababu ya kuhofia kukosa wateja,” alisema
Robert Nyamu, Mkurugenzi wa Delloite, Afrika Mashariki.
Msemaji wa Benki Kuu ya Tanzania,Loy Nabeta hakuwa
tayari kuzungumzia upotevu huo na kusema kuwa ni suala linalohitaji
majadiliano ya kina na utendaji wa ngazi za juu.
Wimbi la wizi wa fedha katika benki lilianza
kupata umaarufu mwaka 2010 na Oktoba 2012 hadi Februari 2013,
inakadiriwa kuwa jumla ya Sh700 milioni zimeibwa katika benki mbalimbali
kwa nyakati tofauti.
Ripoti hiyo ya Uhalifu wa Kiuchumi ya mwaka 2013
iliyotolewa na Kampuni ya Uchunguzi wa Huduma ya Delloite imebaini kuwa
watendaji wa ngazi za juu wanahusika zaidi na uhalifu huo ukilinganisha
na watendaji wa ngazi za chini.
“Wanapofanya uhalifu hujua namna ya kuuficha na
kuujadili na wasimamizi wa ndani bila kubainika.Wanajua mbinu na mifumo
yote ya kifedha na wanatumia fursa hiyo kuiba,” alisema Nyamu.
Watendaji waliotajwa kuhusika zaidi na wizi huo wa
fedha ni wale wa ngazi za juu wakiwamo wakurugenzi watendaji, ofisa
operesheni, wakurugenzi wa fedha, vitengo vya teknolojia na wakuu wa
vitengo wanatumia nafasi zao kufanya uhalifu wa fedha ukilinganisha na
wafanyakazi wa kati na ngazi za chini.
Wizi unaofanyika zaidi katika nchi za Afrika
Mashariki unatajwa kuwa ni wa fedha halali ambao ni zaidi ya asilimia 70
ya uhalifu wa aina zote wa kifedha.
Hata hivyo Nyamu alisema watendaji wa ngazi za
chini wanaweza kufanya uhalifu wa kiasi kikubwa cha fedha iwapo wanajua
namna ya kufanya hivyo.
Mtaalamu wa Uchumi na Mhadhiri wa Chuo cha
usimamizi wa Fedha(IFM), Dk Eliamani Sedoyeka alisema ni kweli kuwa watu
wa ngazi za juu wanatumia nafasi zao kufanya uhalifu wa kifedha kwa
sababu wanaelewa kwa undani mfumo unavyofanya kazi na kutolea mfano i
wizi wa Benki ya StanbicSOURCE: MWANANCHI