Tuesday, 12 February 2008

Baraza Jipya la Mawaziri - Tanzania - 12.Feb. 2008

Rais JK ametangaza Baraza jipya la mawaziri, baada ya kuvunja baraza la mawaziri ya kufuatia Edward Lowasasa kujiuzulu baada ya kukumbwa na kashfa ya Richmond. Akizungumza katika ukumbi wa Tamisemi mjini Dodoma amesema baraza hilo limepunguzwa na kubakia na Mawazirii 26 badala ya 29 wa awali na Manaibu 21 badala ya 31.
Awali kabla ya kutangaza baraza hilo Rais Kikwete alisema kuna mawaziri walioomba kupumzika baada ya kutumikia serikali kwa muda mrefu na watabaki katika kushauri tu. ambao ni Mzee Kingunge Ngombare Mwiru, na Joseph Mungai.
1. (Menejimenti utumishi wa umma) - Hawa Ghasia.
2. (Ofisi ya Rais muungano) - Seif Mohamed Khatib.
3. (Mazingira) - Batilda Burian.
4. (Ofisi ya waziri mkuu utaratibu wa bunge) - Philipo Marmo.
5. (Tamisemi Tawala za mikoa na serikali za mitaa) - Stephen Wasira, naibu Serena Kombani. 6. 6. (Wizara ya mipango na Fedha) - Mustafa Mkulo, manaibu Jeremia Sumari na Omari Yusuph Mzee.
7. (Afya na ustawi wa jamii) - Prof. Mwakyusa, Naibu Asha Kigoda.
8. (Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi) - John Chiligati.
9. (Elimu na mafunzo ya ufundi) - Prof Jumanne Maghembe, Manaibu Gaudensia Kabaka , na Mwantum Mahiza.
10. (Mawasiliano, Sayansi na Technologia) - Shukuru Kawambwa, Naibu Maua Daftari.
11. (Miundo mbinu) - Andrew Chenge, Naibu Milton Mahanga.
12. (Habari Utamaduni na Michezo) - George Huruma Mkuchika, Naibu Joel Bendera.
13. (Kazi Ajira na maendeleo ya Vijana) - Prof Juma Kapuya, Naibu Ezekiel Chibulunje.
14. (Maji na Umwagiliaji) - Prof. Mark Mwandosya, Naibu wake ni Engineer Christopher Chiza. 15. (Kilimo Chakula na Ushirika) - Prof. Peter Msola, Naibu Mathayo David Mathayo.
16. (Maendeleo ya jamii Jinsia na Watoto) - Magreth Sitta, naibu Lucy Nkya.
17. (Maendeleo ya mifugo na uvuvi) - John Pombe Magufuli, Naibu DR. James Wanyancha.
18. (Maliasili na utalii) - Shamsa Mwangunga, Naibu Ezekiel Maige.
19. (Mambo ya Ndani) - Lawrence Masha, naibu Hamis Kagasheki.
20. (Wizara ya Katiba na Sheria) - Mhe. Mathias Chikawe.
21. (Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa) - Bernard Membe, naibu Seif Ally Idi.
22. (Wizara ya Nishati na madini) - Wiliam Ngereja, Naibu ni Adam Malima.
23. (Wizara ya Ulinzi) - Hussein Ally Mwinyi, Naibu Emmanuel Nchimbi.
24. (Wizara Ya Afrika Mashariki) - DR. E Kamala, naibu Mohamed Abdul.
25. (Viwanda na Masoko) - Mary Nagu naibu Cyril Chami.
Wameisha!!!!!!

Thursday, 7 February 2008

BREAKING NEWS!!!!!

Mh.. EDWARD LOWASA (PM)


HABARI TOKA DODOMA SASA HIVI ZINASEMA KUWA SPIKA WA BUNGE MH. SAMWEL SITTA AMETANGAZA KWAMBA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA AMEAMUA KUJIUZULU UWAZIRI MKUU.


MH. SPIKA BAADA YA KUTANGAZA HILO AMESEMA MJADALA WA RIPOTI YA RICHMOND, NA SIO MJADALA WA LOWASSA, NDIO UENDELEE. NA NDICHO KINACHOFANYIKA HIVI SASA HUKO BUNGENI.


HABARI ZAIDI ZINASEMA KWAMBA MH. LOWASSA AMESEMA KWAMBA INGAWA HAJAMTAARIFU JK UAMUZI WAKE HUO, AMEAMUA KUJIWEKA KANDO.


PIA AMEWAELEZA WAANDISHI WA HABARI KWAMBA KAMATI HIYO IMELIAMBIA BUNGE UONGO KWA KUTUMIA ZAIDI MANENO YA UZUSHI. MHESHIMIWA HUYO PIA AMEWEKA BAYANA KWAMBA MPAKA SASA HAJUI NI NANI HASWA ATACHUKUA NAFASI YAKE KAMA RAIS ATARIDHIA OMBI LAKE LA KUJIUZULU WADHIFA WAKE.
BUNGE LIMEAHIRISHWA MPAKA JIONI YA LEO SAA 11 KWA MAAMUZI ZAIDI!
NAWAKILISHA!

Wednesday, 6 February 2008

Mambo ya RICHMOND hayooooooo!!!

Jengo jipya la Bunge Dodoma


Haya sasa ile ripoti ya ubadhilifu wa mamilioni ya fedha za walalahoi sakata la Richmond hii hapa!
Kong'oli hapa http://watanzaniaoslo.blogspot.com/.