Na Beatrice Moses,Mwananchi
Posted Ijumaa,Novemba1 2013 saa 24:0 AM
Posted Ijumaa,Novemba1 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Dar es Salaam. Watu watatu wamekamatwa baada ya kukutwa wakiuza nguo za ndani na soksi kinyume cha sheria, hivyo kuhatarisha afya za wananchi.
Watu hao ambao majina yao yanahifadhiwa
walikamatwa jana wilayani Temeke,Dar es Salaam katika operesheni
inayofanywa na Shirika la Viwango Nchini (TBS) linalolenga kuondoa nguo
za aina hiyo kwenye masoko ya mitumba nchini.
Operesheni hiyo iliyohusisha polisi, iliwafanya wafanyabiashara wengi wa nguo hizo kutimua mbio na kutelekeza bidhaa hizo.
Ofisa Afya wa Manispaa, Leonard Chigalula
alisema,watu hao watashtakiwa katika mahakama za manispaa zinazosimamia
masuala ya afya kwa kuwa nguo hizo zinahatarisha afya za wananchi kwa
kupata maambukizi ya magonjwa ikiwamo fangasi. Ofisa Uhusiano wa TBS,
Roida Andusamile alisisitiza kuwa operesheni hiyo ni endelevu na
kuwasihi wafanyabiashara hao kutafuta biashara nyingine.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI