TASAO TASAO TASAO TASAO TASAO TASAO TASAO TASAO TASAO TASAO TASAO TASAO TASAO TASAO TASAO TASAO
Thursday, 30 May 2013
Wednesday, 29 May 2013
Saturday, 25 May 2013
Friday, 24 May 2013
Tanzania Mtwara gas riots: 'Pregnant woman killed'

Schools and businesses in Mtwara are closed because of the tensions
Residents were angered that the budget, presented in parliament on Wednesday, confirmed the construction of a gas pipeline from Mtwara to Dar es Salaam.
They want a gas processing plant to be built in Mtwara instead.
The 500km (310-mile) pipeline is part of a $1.22bn (£807m) project which will also see the construction of a gas processing plant in Dar es Salaam, the main city of the East African nation.
The security forces were going house-to-house to search for people they thought had been involved in the clashes with police.
Dr Mohamed Kodi at Mtwara's Ligula Referral Hospital told Mwananchi that the woman who died was shot in the stomach. She was seven months pregnant, he said.
Her shooting was also reported in the Kiswahili-language paper Nipache.
The local police commander has refused to comment on the incident.
Correspondents say many men have fled the town because of the crackdown and some women and children have sought shelter in the grounds of Ligula Hospital for safety.
The riots began on Wednesday when the budget confirmed the gas project was going ahead.
Police have been escorting buses travelling into Mtwara to stop them being attacked.
Shops, schools and other businesses in the town remain closed because of the tensions.
There were similar protests in January about the proposed pipeline when the houses of several governing party politicians were burnt down.
Parliament has been temporarily suspended because of the latest trouble.
But President Jakaya Kikwete has said the government will continue with the project despite the protests.
Their demands are not valid because resources belong to the whole country, not one geographical area, he said.
Source: BBC.Com
HALI BADO NI TETE MTWARA
WOULD YOU LIKE TO BE A WRITER, AUTHOR OR COLUMNIST. HERE IS YOUR CHANCE
It is very easy if you are ready for this motivation. Just write and send to us via our
Email: studentsunion.oslo@gmail.com
All of your writings will be published here for the readers.
Thanks
PRO
Thursday, 23 May 2013
Askari-watuhumiwa-kubaka-kumwua-mjamzito-kupora-kuchoma-nyumba-moto

Mbali na unyama huo polisi pia wanadaiwa kuchoma moto nyumba tatu za wananchi katika mtaa wa Magomeni na vibanda vya maduka kadhaa na kupora vitu vilivyomo ndani.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa anasema hali ni shwari na kwamba wananchi watoke nje kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mohamedi Kodi amethibitisha kupokea mwili wa mjamzito ukiwa na tundu tumboni, zinazoaminika kuwa za risasi na hivyo kufanya idadi ya maiti zilizopokelewa hospitalini hapo kufikia mbili na majeruhi 18: “Ni kweli kwa leo tumepokea maiti moja ya mwanamke ambaye ni mjamzito wa
Habari zinadai kuwa mjamzito huyo ameuawa akiwa nyumbani kwake baada ya polisi kuvamia makazi yake.
Huduma za kijamii zimesimama, hakuna maduka yaliyo wazi, hakuna usafiri wa daladala wala pikipiki, mji upo kimya, sauti za milio ya mabomu na bunduki zimetawala, wanajeshi waliovalia sare wameuzingira mji wakiwa katika magari na pikipiki.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari kwa nyakati tofauti wakazi hao wamelalamikia kitendo cha askari wa jeshi la polisi kuingia katika makazi yao, kuwapiga, kuwabaka na kuwapora mali zao:
“Magomeni A hatuna amani askari wanaingia majumbani mwetu wanatupiga na kutunyang’anya simu, yani huku Magomeni hatuna amani kabisa, tumepoteza watoto na hatujui hata waume zetu wako wapi” alisema Paulina Idd na kuongeza: “Majumba yetu yamechomwa moto wanaofanya fujo ni polisi wenyewe halafu wanakuja wanatubaka na kuiba mali zetu halafu tunateseka sisi yaani tumechoka kabisa na serikali yenyewe,” alisema Paulina.
Wakazi wakimbia maeneo yao
Wakazi wa maeneo mbalimbali wamekimbia makazi yao hususani wanawake na watoto na kuhamia hospitali ya rufaa kwa kuhofia usalama wao huku wengi wao wakipotezana na ndugu zao.
Hali hiyo imetokea kufuatia kuwepo kwa milipuko ya mobomu katika maeneo mbalimbali mjini hapa huku huduma za kijamii zikiwa bado zimesitishwa. Hali hiyo imetokea baada ya kusambazwa kwa vipeperushi vilivyokuwa vikihamasisha wananchi wa mkoani hapa kusitisha huduma zote hapo jana ili kusikiliza hotuba ya wizara ya nishati na madini.
Kufuatia hali hiyo imesababisha kifo kwa raia mmoja aliyefahamika kwa jina Karim Shaibu (22) mkazi wa Chikongola ambaye alipigwa risasi wakati wa fujo kati ya jeshi la polisi na wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari mganga mkuu wa mkoa hospitali ya rufaa ya Ligula Dk Sadun Kabuma alithibitisha kupokea kwa kifo hicho ikiwa ni pamoja na majeruhi 17 wakiwemo askari watatu: “Ni kweli jana kuanzia majira ya saa 10 hadi saa 11 nilipokea majeruhi 17 ambapo kati ya hao wamishtuko ni wanawake watano na askari watatu na kijana mwingine ambaye alikuwa na jeraha na katika harakati zan kumwokoa maisha yake alifariki akiwa chumba cha upasuaji,” alisema Dk Kabuma
Wananchi wazungumzia bajeti
Wakizungumzia uwasilishwaji wa hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini wakazi wa hapa wamesema kuwa hawakubaliani na ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kwani mpango huo utawaletea dhuluma: “Mpango wa kusafirishwa kwa gesi asilia hatuna mpango nao kwa wakazi wote wa Mtwara kwa kifupi akina mama wa mtwara hatutaki itoke,” alisema Fatuma Abdallah.
---
Imenukuliwa kutoka wavuti.com kwa msaada wa KARIBU KUSINI Blog
Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/05/mtwara-askari-watuhumiwa-kubaka-kumwua-mjamzito-kupora-kuchoma-nyumba-moto.html#ixzz2U8mSnwWA
TANGAZO MUHIMU
Ndugu
wanaTASAo kama ilivyo ada yetu ule muda wa kuwaaga wenzetu wanaomaliza
masomo mwaka 2013 umewadia. Sherehe zitafanyika siku ya Jumamosi ya
Tarehe 08.06.2013. Sherehe hizi zitafanyika katika Ukumbi wa NORGBERG
KIRKE pale ilipofanyika sherehe ya Uhuru mwezi Desemba 2012. Sherehe
zitaanza saa 12.00 jioni.
Tunaomba sana wote tushiriki kwa wingi.
Sambamba na hilo tunaomba kuwakumbusha michango ya Kiingilio na Ada ya
kila muhula kwa wale ambao hawajatoa. Kwa sababu sherehe hizi
zinaendeshwa kwa michango yaani Kiingilio na Ada tu hakuna mchango zaidi
ya huo. Tunawaomba sana tujitume wenyewe. Unaweza wasilisha mchango
wako moja kwa moja kwa kiongozi yeyote wa TASAO.
Naomba kuwasilisha.
Tunawasalimu pia wale wote mlio huko nyumbani Tanzania. Kila la kheri katika kujenga nchi yetu.
DEZIDERY KAJUNA
PRO
Thursday, 27 September 2012
Saturday, 22 September 2012
Tarehe 22/08/2012 jumuyia ya wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Oslo, Norway wamekuta na kuwakaribisha wanafunzi wapya waliokuja kusoma shahada mbalimbali.
Mhe Rais wa TASAO Mchg. Godrick Lyimo alichakuwa nafasi ya kuwakaribisha wanafunzi hao waliokuja masomoni mwaka huu wa wa masaomo 2012/13. Mhe. Rais aliwapongeza sana wanafunzi hao kwa kupata nafasi ya kuja kusoma Norway, nafasi ambayo sio kila mtu anapata, Mhe Rais pia aliwaambia wanafunzi wapya malengo na madhumuni ya kuwepo kwa chama cha TASAO kuwa ni kujenga umoja wa wanafunzi wa Kitanzania ili waweze kusaidiana wakati wa shida na wa raha, kukaa kama ndugu wakiwa nje ya nchi yao. Mhe Rais aliwaomba wanafunzi wote wapya na wa zamani waendelee kushikamana na kusaidiana kama ndugu maana Tanzania ni moja na watu wake ni wamoja.
Wednesday, 6 April 2011
Mkutano Mkuu wa TASAO na Uchaguzi wa Viongozi Wapya
Friday, 31 December 2010
TAARIFA YA MSIBA
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
Thursday, 22 July 2010
Thursday, 15 July 2010
Sunday, 27 June 2010
HAVE YOU EVER VISITED RUAHA NATIONAL PARK? HERE ARE SOME CLUES


Tuesday, 22 June 2010
Friday, 11 June 2010
Bajeti ya Kilimo Kwanza
11th June 2010
- Kodi zake kibao zafutwa
- Za bia, sigara, magari juu
- Petroli, dizeli zapona

Serikali imetangaza bajeti mpya ya mwaka wa fedha wa 2010/11 ambayo imejielekeza kusaidia zaidi wakulima na wafugaji kwa kuwaondolea kodi mbalimbali, lakini imeendelea na jadi yake ya kuongeza kodi kwenye bia, vinywaji baridi, mvinyo, pombe kali, sigara na usajili wa magari.
Akiwasilisha bajeti hiyo bungeji jana jioni, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mukulo, alisema ongezeko la kodi hizo ni la asilimia nane kiwango ambacho hakizidi mfumuko wa bei.
Katika bajeti hiyo, mafuta ya petroli na bidhaa zake zote kodi zake hazijaguwa. Hata hivyo kuna punguzo mafuta ya kuendesha mitambo kutoka Sh. 97 hadi 80 kwa lita.
Ongezeko la viwango hivyo na vile vya zamani kwenye mabano ni vinywaji baridi Sh. 63 kwa lita (Sh. 58) na bia inayotengenezwa na nafaka ya hapa nchini na ambayo haijaoteshwa Sh. 226 kwa lita (Sh. 209) wakati bia nyingine zote zimepanda kutoka Sh. 354 kufikia Sh 382 kwa lita.
Alisema mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25 itakuwa Sh. 1,223 kwa lita (Sh 1,132) na vinywaji vikali itakuwa Sh. 1,812 kwa lita (Sh. 1,678).
Kwa upande wa sigara, Mkulo alisema zile zisizokuwa na kichungi na zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75 itakuwa Sh. 6,209 kwa sigara 1,000 (Sh. 5,749).
Kwa sigara zenye kichungi na zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, itakuwa Sh 14,649 (13,564).
Alisema sigara nyingine zenye sifa tofauti na hizo, itakuwa Sh. 26,604 kwa sigara 1,000 (Sh. 24,633).
Wakati huo tumbaku ambayo ipo tayari kwa utengezaji wa sigara itakuwa Sh. 13,436 kwa kilo (12,441 na ushuru wa cigar unabaki kuwa asilimia 30.
“Hatua hizi katika ushuru wa bidhaa kwa pamoja zinatarajiwa kupunguza mapato ya serikali kwa kiasi cha Sh. bilioni 20.042,” alisema.
Mkulo alisema serikali imesamehe kodi ya majengo kwa nyumba wanamoishi wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60, ambao hali zao kiuchumi haziwawezeshi kulipa kodi hiyo.
“Hata hivyo msamaha huo utatolewa kwa wale watakaothibitishwa na uongozi katika serikali za mitaa kuwa kweli hawana uwezo wa kulipa kodi husika,” alisema.
Pia alisema kiwango cha kutoza ushuru wa mazao shambani kitakuwa kati ya asilimia 3 na 5 ya bei ya kuuza mazao mashambani, ili kuzipa fursa halmashauri na serikali za mitaa kutoza ushuru huo kulingana na uwezo na rasilimali zilizopo.
Ada ya usajili wa magari na pikipiki
Alisema usajili wa magari unatapanda kutoka Sh. 120,000 hadi Sh. 150,000 wakati pikipiki itakuwa Sh. 45,000 ikilinganisha na Sh 35,000 za awali.
Mkulo alisema hatua hizo zitaongeza mapato ya serikali kwa Sh. bilioni 3.19
Ada ya mwaka ya leseni
Kwa upande wa ada ya mwaka ya leseni za magari itakuwa Sh. 50,000 badala ya Sh. 30,000 kwa gari lenye ujazo wa injini 0-500cc.
Gari lenye ujazo wa injini 501 hadi 1,500cc, itapanda kutoka Sh. 50,000 hadi kufikia Sh. 100,000 wakati lenye ujazo wa kati ya 1501-2,500 itakuwa Sh 150,000 badala ya Sh 100,000.
Kwa upande wa gari lenye ujazo wa injini zaidi ya 2,501 ada itakuwa Sh 200,000 badala ya Sh. 150,000 ya sasa.
“Hatua hizi katika kuongeza viwango vya ada ya mwaka ya leseni za magari kwa pamoja zinatarajiwa kuongeza mapato ya serikali kwa kiasi cha Sh. bilioni 16.981,” alisema.
Usafirishaji korosho
Mkulo alisema kutakuwa na ongezeko la ushuru wa kusafirisha korosho ghafi kutoka asilimia 10 ya sasa hadi 15 (ama Dola 160 za Marekani) kwa tani moja.
Alisema lengo la ongezeko hilo ni kulinda viwanda, kuongeza ubora na thamani ya korosho na kukuza ajira kwa wananchi.
Kwa mujibu wa Mkulo hatua hiyo inatarajiwa kuongeza mapato ya serikali kwa Sh bilioni 2.613.
Michezo ya kuhabatisha
Mkulo alisema kiwango cha kodi inayotozwa kwenye mashine za michezo ya kubahatisha itaongezeka kutoka Sh. 16,000 hadi 32,000 wakati kodi ya kiwango cha asilimia 13 ya mapato itatozwa katika mashine ya tombola, hivyo kuongeza mapato ya serikali kwa Sh. bilioni 0.5.
Misamaha wa kodi
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika usafirishaji wa mazao ya kilimo kutoka shambani hadi kwenye viwanda vya usindikaji kwa wakulima wenye kilimo cha mkataba wa miwa, mkongwe na chai imesamehewa.
Kodi nyingine iliyosamehewa ni VAT katika mashine na vifaa vya vya kukusanya, kusafirisha na kusindika maziwa ili kuhamasisha uwekezaji katika sekta ndogo ya maziwa na kuboresha kipato kwa wananchi.
Mashine na vifaa vitakavyohusika katika msamaha huo ni vifaa maalum vya kubebea maziwa, pampu maalum za kusukumia maziwa na bomba maalum la kupitishia maziwa kwenye viwanda vya usindikaji.
Vifaa vingine vilivyopata msamaha huo ni kompresa maalum zinazotumika kwenye vifaa vya kupoza maziwa, matanki ya kuhifadhia maziwa gari maalum lenye kifaa cha kupoza na kusafirisha maziwa.
Vingine ni mtambo maalum wa kuchemsha maziwa ili kutoa siagi, vifaa maalum vya kupoza na kutengeneza ubaridi na kifaa maalum cha kukandamiza na kukamua maji ili kuzalisha jibini.
Mkulo alisema msamaha mwingine umetolewa kwenye mashudu kwa ajili ya chakula cha mifugo.
Hatua hiyo inalenga kuhamasisha ufugaji bora na kuwawezesha wakulima wa mbegu za mafuta kupata bei yenye tija kwa mauzo ya bidhaa hiyo.
Pia, serikali imetoa unafuu maalum wa VAT kwa vifaa vinavyouzwa kwa watalaam wa mifugo waliosajiliwa.
Vitu vingine vilivyosamehewa VAT ni zana za kilimo kama kivuna nafaka, pick up balers, mashinde ya kufunga majani ya ng’ombe (hay making machinery) na mowers vinavyotumika mahsusi katika uzalishaji wa kilimo na mifugo.
Sekta ya kilimo cha maua nayo imenufaika na msamaha wa VAT kwa ufarishaji wa maua kwa ndege kwenda nje ya nchi, kwa mabanda (green house) yanayotumika katika kilimo cha maua.
Bajeti hiyo inaonyesha pia kutoa unafuu maalum wa VAT katika uuzaji wa bidhaa na huduma zinazotolewa kwa wakulima waliosajiliwa ama mashamba ya vyama vya ushirika na ujenzi wa miundombinu ya mashamba.
Miundombinu hiyo ni pamoja na mitaro ya umwagiliaji, barabara za mashambani, ujenzi wa maghala au huduma nyingine zinazofanana na hizo.
Pia msamaha wa VAT umetolewa kwa huduma za kuzalisha mifugo kwa njia ya kupandisha mifugo na kutumia mashine maalum za kuzalishia ama kutotolea vifaranga.
Mkulo alisema ili kuhamasisha uwekezaji na uzalishaji katika sekta ya viwanda nchini, unafuu maalum wa VAT umetolewa kwa waendelezaji wa maeneo yenye uwekezaji kwenye bidhaa za kuuza nje yaani EPZ na SEZ.
Mkulo alisema kutakuwa na tozo la VAT kwa asilimia sifuri katika usindikaji na uzalishaji wa mafuta ya kula kwa wazalishaji wanaotumia mbegu za mafuta zinazozalishwa hapa nchini.
Alisema VAT imesamehewa katika vifungashio vya juisi za matunda na bidhaa za maziwa.
“Hatua hii inalenga katika kupunguza gharama za uzalishaji na kuboresha thamani ya bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda vya juisi na maziwa hapa nchini,” alisema.
Mkulo alisema serikali imerejesha utaratibu wa kutambua baadhi ya vifaa kama bidhaa za mtaji kwa wawekezaji ili kuvipa nafuu ya kodi.
Hata hivyo, alisema serikali itaunda kamati maalum ya kushughulikia suala hilo, ili kudhibiti matumizi mabaya ya utaratibu huo yanayoweza kuvujisha mapato.
Alisema hatua hizo zinazohusu VAT zitasababisha kupungua kwa mapato ya serikali kwa kiasi cha Sh. bilioni 2.39.
Kuhusu sheria ya kodi ya mapato sura 332, Mkulo alitoa kauli ya kurekebisha kifungu cha 11 cha sheria hiyo ili kuweka wigo wa ukomo wa maeneo ya uchimbaji wa madini.
Alisema nia ni kudhibiti gharama zinazotakiwa kutolewa katika kukokotoa faida, itakayotozwa kodi ya mapato kwa eneo husika.
Pia kutokana na kuwepo biashara nyingi zinazofanywa na watu wasiokuwa na namba za utambulisho wa mlipa kodi (Tin), alipendekeza kodi ya zuio inayozuiwa na serikali kwa wauzaji wa bidhaa na watoa huduma wasiokuwa na Tin, izuiwe.
Mkulo alitangaza punguzo la ushuru wa bidhaa kwenye mafuta mazito ya kuendesha mitambo kutoka Sh. 97 hadi 80 ili kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa hapa nchini.
Alisema hatua hiyo imezingatia ridhaa ya serikali kukuza viwanda, ajira na mapato ya ndani.
Pia alisema punguzo hilo limezingatia makubaliano ya serikali na wenye viwanda kupunguza ushuru huo na hatimaye kuufuta katika kipindi cha miaka mitatu.
Waziri huyo aliomba Bunge liidhinishe Sh. milioni 11,609,557 kati ya hizo matumizi ya kawaida ni Sh. milioni 7,790,506 na za maendeleo ni Sh. milioni 3,819,051.


