Thursday, 29 August 2013

Moto wateketeza Baa ya samaki Samaki Mbezi Beach

                            
Moto mkubwa umeteketeza jengo la baa ya Samaki Samaki Mbezi Beach
Jijini Dar Es Salaam na kuleta taharuki kwa wamiliki wa majengo jirani jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa mashuhuda,moto huo ulioanza majira ya saa tano umelipuka gafla na kusambaa mara baada ya tingatinga lililokuwa likibomoa kupisha njia ya ujenzi wa bomba kuu la maji toka Ruvu chini hadi jijini Dar es salaam kubomoa sehemu ya mbele ya jengo hilo huku wakilalamikia uchelewaji wa vikosi vya zimamoto na uokoaji

Hata hivyo meneja wa jengo hilo aliyedai kuwepo hapo wakati wa ubomoaji huo amesema chanzo ni ubishi wa opareta wa tingatinga aliyeombwa kubomoa kwa umakini kabla ya tukio kutokana na uhalisia wa jengo kujengwa kwa makuti, nyasi, mbao na miti mikavu huku likiwa na mtandao wa nyaya nyingi za umeme.

Itv imeshuhudia tingatinga hilo likiendelea kubomoa maeneo ya Mbezi beach huku baadhi ya wamiliki wa majengo yanayobomolewa kupisha ujenzi wa bomba hilo wakiiomba serikali kuangalia kwa jicho la upendeleo baadhi ya wamilki wa majengo ambao wanatambulika kisheria wakiutaja kuwa ni uzembe unaotokana na watendaji wa serikali wasiokuwa waaminifu kwa kutoa hati na vibari vya ujenzi.

source: ITV