Thursday, 29 August 2013

Wabunge wa Tanzania wametoka nje ya kikao EALA


                            
 Kikao cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA),kilivunjika kwa mara ya pili baada ya Wabunge wa
Tanzania, kutoka ndani ya ukumbi wakipinga kanuni kuvunjwa.
Baada ya wabunge wa Tanzania kutoka nje, Spika wa Bunge hilo, Margareth Zziwa aliahirisha Bunge kwa dakika 15 ili kuweka mambo sawa, lakini jitihada za kuwashawishi ziligonga mwamba na kuamua kuahirisha Bunge hadi leo.
Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa wenzetu, kudharau kiti cha Spika na kutaka kutoa hoja na kujadiliwa bila kufuata kanuni, sasa tumeona ni vizuri na sisi kwa kupinga kuvunjwa kanuni, tutoke ili kuonyesha tunapinga mchezo huu,haya yalikuwa ni maelezo ya mmoja wa wabunge wa Bunge hilo Abdullah Ali Hassan Mwinyi.
Mbunge wa Kenya, Peter Mathuki alitaka hoja yake ya kutaka utaratibu wa kufanyika kwa vikao vya bunge hilo kwa mzunguko ijadiliwe kitu ambacho kilipingwa na wabunge wa Tanzania, Hata hivyo Muthuki, juzi aliungwa mkono na nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), isipokuwa Tanzania.
Jana aliwasilisha hoja hiyo kwa kufuata utaratibu lakini haikujadiliwa baada ya wabunge wa Tanzania kutoka nje.
Katika hoja hiyo, msimamo wa wabunge wa Tanzania na Kamati ya Uongozi ya Bunge ni kuwa vikao vyote vifanyike katika ukumbi wa Bunge, Arusha baada ya Ukumbi huo kukamilika kujengwa.
                          
Mh. Abdullah Ali Hassan Mwinyi alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari
Source: ITV