Friday, 30 August 2013

Wizi mitandaoni wamkera Makamba


Na Hamida Shariff  (email the author)

Posted  Alhamisi,Agosti29  2013  saa 21:55 PM
Kwa ufupi
Makamba aliyasema hayo jana mjini hapa wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wadau mbalimbali wa taasisi za fedha ikiwepo Benki Kuu ya Tanzania(BOT).


Morogoro.Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia,mitandao imekuwa ikihusika hivyo ni lazima iwe salama kwa kudhibiti wizi unaoendelea kufanyika nchini.
Makamba aliyasema hayo jana mjini hapa wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wadau mbalimbali wa taasisi za fedha ikiwepo Benki Kuu ya Tanzania(BOT), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Mifuko ya hifadhi ya jamii, Ofisi ya mkaguzi, maafisa kutoka taasisi na ofisi za Serikali pamoja na wadau wa mitandao ya simu .
Mafunzo hayo yalifadhiliwa na Shirika la ISACA Tanzania Chapter linaloshughulikia wizi wa mitandaoni kwa nchi za Afrika Mashariki lenye makao makuu Marekani kwa kushirikiana na Kampuni ya Norway Registerd Development (NRD) ambayo inashughulika na usalama wa mitandao.

source : Mwananchi