Friday, 30 August 2013

Wazawa wanufaike na rasilimali



Na Geofrey Nyang’oro  (email the author)

Posted  Alhamisi,Agosti29  2013  saa 21:49 PM
Kwa ufupi
Akitoa maoni yake katika mchakato huo, Percival Lwoga alisema Katiba Mpya itamke bayana kuwa suala la ardhi ni mali ya mzawa na hata inapogundulika ni maliasili katiba ionyeshe namna atakavyonufaika nayo.


Iringa.Wajumbe wanaoshiriki mkutano wa kukusanya maoni ya Rasimu ya Katiba uliondaliwa na Mwavuli wa Asasi za Kiraia Mkoani Iringa (ICSO) wamependekeza rasilimali za Taifa zitumike kunufaisha wakazi wa maeneo husika. Akitoa maoni yake katika mchakato huo, Percival Lwoga alisema Katiba Mpya itamke bayana kuwa suala la ardhi ni mali ya mzawa na hata inapogundulika ni maliasili katiba ionyeshe namna atakavyonufaika nayo. Hatua hiyo itaondoa migogoro ya mara kwa mara inayowakumba Watanzania pindi inapobainika katika maeneo wanayoishi kuna maliasili ikiwemo madini.