Wednesday, 28 August 2013

Sudan, Somalia zaomba uanachama Jumuiya EAC

Na Mussa Juma  (email the author)

Posted  Jumanne,Agosti27  2013  saa 22:24 PM
Kwa ufupi
Alisema kikao cha baraza la mawaziri kinatarajia kupokea ripoti kuhusu maombi hayo, ambapo tayari timu ya maofisa wa jumuiya hiyo ilikwenda Sudan Kusini kutazama kama ina sifa za kujiunga na jumuiya hiyo.

Arusha. Nchi za Sudani Kusini na Somalia, zimeomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki(EAC) na tayari mchakato wa kupitia maombi hayo umeanza.
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Dk Richard Sezibera alitoa taarifa hiyo jana katika kikao na waandishi wa habari, wakati akielezea kuanza kikao cha baraza la mawaziri wa jumuiya hiyo.
Alisema kikao cha baraza la mawaziri kinatarajia kupokea ripoti kuhusu maombi hayo, ambapo tayari timu ya maofisa wa jumuiya hiyo ilikwenda Sudan Kusini kutazama kama ina sifa za kujiunga na jumuiya hiyo.
Alisema kwa upande wa Somalia, baraza hilo linatarajia kuridhia uamuzi wa Sekretarieti ya jumuiya ya kutuma maofisa wake kwenda Somalia kutazama kama ipo tayari kujiunga .
Aidha alisema hadi nchi hizo kukubaliwa kuwa mwanachama kuna mchakato mrefu zitapitia.

source: Mwanachi