Kwa ufupi
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamalaka ya Kodi
Tanzania (TRA), Rished Bade, ambaye kwa jana alikuwa mkuu wa msafara,
alisema ujumbe wake utakuwa na mazungumza na wenzao wa Zambia kwa nia ya
kuboresha utendaji na kuimarisha uhusiano.
Mbeya. Tanzania na Zambia
zimeanza mazungumzo maalumu ya kutafuta mbinu za kuboresha utendaji kazi
wa kusafirisha mizigo kwenye mpaka wa nchi hizo, uliopo Tunduma.
Tayari, ujumbe wa zaidi ya watu 20 kutoka Wizara
za Uchukuzi, Fedha, Mambo ya Ndani na wadau wa usafirishaji waliwasili
jijini Mbeya tangu juzi, jana walikwenda Tunduma mpakani mwa Tanzania na
Zambia kujionea utendaji ulivyo kwa upande wa Tanzania.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamalaka ya Kodi Tanzania
(TRA), Rished Bade, ambaye kwa jana alikuwa mkuu wa msafara, alisema
ujumbe wake utakuwa na mazungumza na wenzao wa Zambia kwa nia ya
kuboresha utendaji na kuimarisha uhusiano.
Bade alisema baada ya ujumbe, kitafuata kikao cha
makatibu wakuu wa wizara zote zinazohusika za Tanzania na zile za
Zambia kitakachofanyika Oktoba 3.
“Pamoja na mengineyo, lengo kubwa ni kuandaa
taratibu za kuanza ujenzi wa kituo kimoja cha mpakani kwa magari yote
ya Zambia na Tanzania ( One Stop Boarder Post), ili kuondokana na
usumbufu wa sasa,” alisema.
Alisema tayari ujumbe wa Zambia walikuwa wakijiandaa kwenye Mji wa Nakonde nchini Zambia, kabla ya kukutana kuanzia kesho.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI