Na Hakimu Mwafongo, Mwanananchi
Posted Jumatatu,Oktoba28 2013 saa 11:1 AM
Posted Jumatatu,Oktoba28 2013 saa 11:1 AM
Dola na mamlaka nyingi za nchi, zinaendelea kukandamiza vyombo vya habari na kudidimiza haki ya watu kupata habari.
Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri, Absalom Kibanda, baada ya kutembelea mnara wa kumbukumbu ya
mauaji ya mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel ten
mkoani Iringa, Daud Mwangosi.
Mnara huo umejengwa katika Kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi.
Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni
ya New Habari, alisema wanahabari mkoani Iringa wametembelea eneo hilo,
ili kuonyesha mshikamano wao katika kuihabarisha jamii.
Pia alisema wahariri ambao hawakupata fursa ya
kufika eneo hilo wakati wa mauaji ya mwandishi huyo, wameweza kuipata
kumkumbuka ya Mwangosi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi
wa Habari wa Mkoa wa Iringa.
Alisema jambo walilofanya linatoa ujumbe kwa mamlaka na vyombo vya dola kutambua haki ya uhuru wa habari na kujieleza.
“Wadau wote wa habari wanatakiwa kutambua kuwa
uhuru wa habari wa kujieleza na kuhabarisha ni haki ya msingi ya kila
Mtanzania ingawa mamlaka zikandamiza haki hiyo,” alisema.
Mjumbe wa jukwaa hilo, Theophil Makunga, alisema
Mwangosi aliuawa akimtetea mwandishi mwenzake wa Gazeti la Nipashe,
Godfrey Mushi aliyekuwa akipigwa na askari katika vurugu zilizotokea
katika mikutano ya Chadema, kijijini Nyololo.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI