Na Frederick Katulanda, Mwananchi
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013 saa 24:0 AM
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Mwanza. Jeshi la Polisi
limemnasa mtu mwingine na kumuunganisha katika kesi ya kukutwa na
kiganja cha mkono wa binadamu. Kukamatwa kwa mtu huyo, kunafanya
watuhumiwa waliotiwa nguvuni mpaka sasa kufikia wanne.
Taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi
zilizothibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi, Joseph Konyo zimesema
mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuwa ni mtumishi wa Serikali Idara ya Afya,
ndiye aliyefanikisha kupatikana kwa kiganja hicho.
“Tumefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mwingine, kwa
sasa tunafanya uchunguzi, siwezi kuthibitisha kama ni mtumishi wa
Serikali au la,” alisema Konyo.
Watuhumiwa wengine watatu walinaswa Novemba 28
mwaka huu eneo la Ziwani, Uwanja wa Ndege wa Mwanza wakiwa katika
jitihada za kuuza mkono huo baada ya kuwekewa mtego na polisi.
Konyo alisema kazi ya kuwakamata watuhumiwa wengine kuhusiana na tukio hilo inaendelea.
“Kufanikiwa kumnasa mtuhumiwa huyu ni mafanikio
makubwa kwa vile inaonekana ndiye anafahamu kila kitu kuhusu kiganja
hicho kilipatikana wapi na kwa namna gani,” alisema Konyo.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI