Na Tausi Ally, Mwananchi
Posted Jumatatu,Oktoba28 2013 saa 10:34 AM
Posted Jumatatu,Oktoba28 2013 saa 10:34 AM
Dar es Salaam. Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, leo itatoa hukumu kuhusu kesi ya
utapeli inayomkabili mwanasiasa mkongwe, Arcado Ntagazwa na wenzake
wawili.
Ntagazwa aliwahi kuwa waziri wa Serikali. Hukumu
hiyo imeahirishwa mara mbili, mara ya kwanza ilikuwa Oktoba 17,mwaka huu
ambapo Hakimu Mkazi Geni Dudu, alisema alikuwa bado anaiandika.
Mara ya pili ilikuwa Ijumaa iliyopita ambapo hakimu huyo alisema alikuwa anaihakiki hukumu.
Siku hiyo ya Ijumaa Ntagazwa, alifika mahakama saa 2.00 asubuhi akionekana mwenye kujiamini.
Alioonekana akiongea na waandishi wa habari nje
ya mahakama na baadaye kupiga nao picha kabla ya kwenda mahakamani
kusikiliza hatima yake.
Ntagazwa, mwanaye Webhale Ntagazwa na mshirika
wake, Senator Miselya (60), wanakabiliwa na kesi ya utapeli kwa
kujipatia kwa njia ya udanganyifu, fulana 5,000 na kofia idadi kama
hiyo za kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Sare hizo zinadaiwa kuwa na thamani ya Sh 74,950,000, mali ya Noel Severe.
Wakati wa usikilizaji wa awali wa kesi hiyo, Ntagazwa alikanusha madai dhidi yake.
Hata hivyo katika ushahidi wake wa utetezi,
mshtakiwa alikubali kuwa alikuwa hajalipa Sh 74, 950,000 kwa ajili
ya vifaa hivyo.
Pia alidai kuwa aliwadanganya polisi kwa kukubali shtaka hilo mbele yao.
Alidai kuwa alikubali shtaka hilo ili kukwepa kusumbuliwa.
Washtakiwa katika kesi hiyo pia walikubali kupokea fulana na kofia lakini walirushiana mpira kuhusu malipo ya fedha hizo.
SOURCE: MWANANCHI
Washtakiwa hao walilazimika kupanda kizimbani kujitetea baada ya mahakama kuwaona kuwa wana kesi ya kujibu.
Upande wa mashtaka uliwaita mashahidi watano.
Washtakiwa katika kesi hiyo, wanadaiwa kutenda makosa hayo Oktoba 24, 2009, katika maeneo ya Mikoroshini.
Inadaiwa kuwa walimuahidi Severe kwamba wangemlipa kiasi hicho cha fedha ndani ya mwezi mmoja huku wakijuaSOURCE: MWANANCHI