Mahakama
ya rufaa imeanza kupitia hukumu ya mwanamuziki maarufu nchini mwenye
asili ya jamhuri ya kidemokrasia ya congo DRC Nguza Viking maarufu
kama Babu seya na mwanawe Johnson Nguza maarufu kama Papii kocha.
Mapitio hayo yanafanywa na jopo la majaji watatu
wakiongozwa na Mh Nathali Kimaro amboa ndio waliotoa hukumu Februari
2010 kwa upande wa waleta maombi wakiongozwa na wakili Mabetre Marando
wamewasilisha mahakamani hapo mambo sita ambayo wangepedwa mahakama hiyo
iyaangaliye kwa makini,ambapo moja ya mambo hayo ni pamoja na kuwa
wakati wa usikilizwaji wa kesi mashahidu muhimu hawakuitwa kutoa ushaidi
wao.
Aidha wanataka ushaidi wa watoto uliotolewe katika
kesi hiyo uondolewe katika kumbukumbu kwa sababu haukufuta taratibu na
vigezo vya matwakwa ya sheria ya ushaidi pia wamesema kuwa katika
ushaidi uliotolewa ulionyesha kuwa katika nyumba ya babu seya
kulikuwa na mlango wa siri lakini mahakama ilipokwenda hapo mlango huo
haukuonekana.
Kwa upande wa serikali kupitia wakili wake
mwandamizi jackson burashi wameiomba mahakma hiyo kutupilia mbali
shauri hilo kutokana na ukweli kuwa yapo hapo kinyume na sheria na
yameletwa kama rufaa na siyo mapitio.
Aidha akaongeza kuwa maombi hayo hayajakidhi
viwango vya sababu za mapitio kwa kuwa maombi hayo yalipaswa kuonyesha
kuwa kosa limetendeka na haki ya mleta rufaa imepotea. Baada ya maelezo
ya pande zote mbili mahakama ikasema itatoa maamuazi baada ya kupitia
maelezo ya pande zote mbili
Babu Seya na mwanaye papii kocha wanaendelea
kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hati ya
makosa ya kunajisi na kulawiti watoto wadogo kupitia huku iliyotolewa
na mahakama ya hakimu mkazi kisutu mwaka 2004 ambapo walihkumiwa
kifungo cha maisha.
SOURCE: IPPMEDIA