Watu
wawili wanaodaiwa kuhusishwa na vitendo vya kigaidi wameuawa kwa
kupigwa risasi wakati kundi hilo lilipokuwa msikitini huku wafuasi wake
wakiwa na silaha za moto na baridi walipokuwa wakijibizana kwa kutumia
silaha mbali mbali ndipo askari walipowahi kuwashambulia viongozi wa
kundi hilo kisha kuwanyang'anya silaha zao ili kuepuka madhara makubwa
zaidi.
Mkuu
wa mkoa wa Tanga luteni mstaafu Chiku Gallawa amesema tukio hilo
limetokea katika kijiji cha Kimamba kilichopo kata ya Negero wilayani
Kilindi wakati kundi hilo lilipokuwa limejiandaa kujibu mashambulizi ya
askari msikitini kwa kuwa na silaha aina ya bunduki na mapanga ndipo
viongozi hao waliposhambuliwa ambapo mmoja alifariki papo hapo huku
mwingine akifariki hospitali ya wilaya.
SOURCE: ITV