Na Tausi Ally, Mwananchi
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013 saa 24:0 AM
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Alidai kuwa ushahidi wa watoto hao ulichukuliwa bila ya kufuatwa kwa taratibu za uchukuaji wa ushahidi wa mtoto.
Dar es Salaam. Mwanamuziki
Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na wanawe kupitia Wakili Mabere
Marando wameiomba Mahakama ya Rufaa, ifanye marejeo kuhusu hukumu
iliyoitoa na ifute ushahidi uliowatia hatiani na adhabu ya kifungo cha
maisha jela wanayoitumikia.
Marando aliliwasilisha ombi hilo, kwa takribani saa 2 mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo .
Jopo hilo linaongozwa na Jaji Nathalia Kimaro, akisaidiana na Jaji Mbarouk Mbarouk na Jaji Salum Massati.
Wakili huyo alisema wateja wake wanaoomba mahakama ifute ushahidi uliowatia hatiani washtakiwa na badala yake iwaachie huru.
Upande wa Mkurugenzi wa Mashtaka, uliwakilishwa na
mawakili Jacksoni Mlaki, Angaza Mwaipopo, Emakulata Banzi, Joseph Pande
na Apimack Mbarouk.
Hata hivyo mawakili hao waandamizi wa Serikali,
waliyapinga maombi hayo kuhusu marejeo kwa madai kuwa yamepelekwa
mahakamani bila usahihi.
Marando alidai kuwa mahakama iliteleza katika
kutoa uamuzi uliowatia hatiani na kuwafunga maisha Babu Seya na watoto
wake na kwamba kuteleza huko kunaonekana wazi wazi.
Alifafanua kuwa wakati wakifanya majumuisho ya
kesi hiyo, mahakama ilijiridhirisha kuwa kulikuwa na makosa katika
kupokea ushahidi wa watoto wanaodaiwa kufanyiwa vitendo hivyo.
Alidai kuwa ushahidi wa watoto hao ulichukuliwa bila ya kufuatwa kwa taratibu za uchukuaji wa ushahidi wa mtoto.
Alisema kwa msingi huo, ushahidi huo ulipaswa kufutwa.
“Katika hukumu yenu mlikubaliana na sisi kuwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kupokea ushahidi wa watoto ,
ila mlisema hiyo si hoja maadam kuna ushahidi unaounga mkono ushahidi
huo ni bora,”alilalamika Marando.
Alieleza kuwa mtoto mdogo anapotoa ushahidi licha
ya tahadhari, ana uwezo wa kutambua zuri na baya na kwamba lazima
ushahidi wake uwekwe kwenye kumbukumbu ya maandishi na kwamba
usipoonekana ushahidi wote ni batili na uondolewe.
SOURCE: MWANACHI
Aliendelea kueleza kuwa kwenye hukumu wanayoilalamikia, anaiomba
mahakama ijisikie kubadili uamuzi wa kuwafunga maisha wateja wake.
“Tuanaomba ushahidi wa wale watoto ufutwe, uondolewe mahakamani na washtakiwa waachiwe huru,”alisisitiza.
Upande wa mashtaka ulipaswa kuwaita mashahidi hao
lakini nyie majaji katika hukumu yenu mlisema upande wa mashtaka
uanahiari ya kumwita shahidi wanayemtaka wao.
SOURCE: MWANACHI