Na Mwinyi Sadalla na Beatrice Moses, Mwananchi
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013 saa 24:0 AM
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Mapema mwili wa Balozi Sepetu uliagwa na
waombolezaji wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi
na viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama vya siasa shughuli ambayo
ilifanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo eneo
la Kikwajuni katika Manispaa ya Zanzibar kabla ya misa maalumu
iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph katika Mtaa wa Shangani.
Zanzibar/Dar. Rais wa
Zanzibar,Dk Ali Mohammed Shein, jana aliwaongoza mamia ya waombolezaji
katika maziko ya mwanasiasa na mwanadiplomasia mkongwe Marehemu
Balozi Issack Abraham Sepetu (71),aliyezikwa katika Kijiji cha Mbuzini,Mkoa wa Kusini Unguja jana Alasiri.
Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni
pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed
Gharib Bilal pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa
Kitaifa ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Mapema mwili wa Balozi Sepetu uliagwa na
waombolezaji wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi
na viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama vya siasa shughuli ambayo
ilifanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo eneo
la Kikwajuni katika Manispaa ya Zanzibar kabla ya misa maalumu
iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph katika Mtaa wa Shangani.
Watoto wa marehemu, Amani,Mkusa, Wema na wengineo
walikuwapo katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na Balozi mstaafu, Ali
Abeid Karume, ambaye alisema marehemu ameacha pengo kubwa katika jamii
kwani alikuwa kiongozi makini na mzalendo aliyelipenda taifa lake.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Vuai Ali
Vuai,alimwelezea marehemu kama mwasisi wa mazungumzo ya kutafuta mwafaka
wa kisiasa Zanzibar wakati juhudi hizo zilipoanza mara ya kwanza baada
ya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi visiwani mwaka 1995 kupitia
kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Chifu Emeka Anyaoku.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI