Na Brand Nelson, Mwananchi
Posted Jumatano,Oktoba30 2013 saa 24:0 AM

Kwa ufupi
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip
Mulugo alitoa agizo hilo jana alipotembelea shule hiyo kujua ukweli,
ambapo pia aliagiza wanafunzi sita wa kidato cha tatu walioshirikiana na
mwalimu huyo kusimamishwa masomo kwa kipindi kisichojulikana ili
kupisha uchunguzi
Mbeya.Serikali imewaagiza
polisi mkoani Mbeya kumsaka mahali popote alipo aliyekuwa Mkuu wa Shule
ya Sekondari Nazarene iliyopo jijini hapa(jina tunalo) kwa madai ya
kufanya udanganyifu wakati wa Mitihani ya Taifa ya Kidato cha pili
akiwashirikisha wanafunzi sita wa kidato cha tatu Oktoba 7 mwaka
huu.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo alitoa agizo hilo jana alipotembelea shule hiyo kujua ukweli, ambapo pia aliagiza wanafunzi sita wa kidato cha tatu walioshirikiana na mwalimu huyo kusimamishwa masomo kwa kipindi kisichojulikana ili kupisha uchunguzi.Ilielezwa kwamba wanafunzi hao walikamatwa wakifanya mitihani ya kidato cha pili kwa kutumia majina bandia ambayo walidai walipewa na mkuu wao wa shule na wala hayakuwa ya wanafunzi wa shule hiyo.
Baada ya wasimamizi wa mitihani kuwakamata wanafunzi hao, ilielezwa kwamba mkuu wa shule hiyo ambayo inamilikiwa na Kanisa la Nazarene la Kenya alitoweka na hadi sasa hajulikani aliko.
SOURCE: MWANANCHI