Kwa ufupi
Hadi umauti unamkuta, Balozi Sepetu alikuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega
Uchumi Zanzibar na Mjumbe wa Bunge la Afrika Mashariki
Dar es Salaam. Balozi wa zamani
wa Tanzania nchini Urusi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Isaack
Sepetu, amefariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya TMJ Mikocheni,
jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa.
Habari zilizopatikana jana zilisema marehemu
Sepetu ambaye ni baba mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema, alilazwa
hospitalini akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na kupooza.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda Zanzibar leo kwa ajili ya taratibu zote za mazishi
Hadi umauti unamkuta, Balozi Sepetu alikuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega
Uchumi Zanzibar na Mjumbe wa Bunge la Afrika Mashariki.
Sepetu aliyetumia sehemu ya maisha yake Zanzibar,
alimaliza masomo yake 1963 na kupata mafunzo mbalimbali nchini Ujerumani
kabla ya kuteuliwa kuwa balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI