Na Waandishi Wetu,Mwananchi
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013 saa 24:0 AM
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Madai hayo yalitolewa jana na shahidi wa 13 katika
kesi kuhusu utoroshaji wa wanyama hai kupitia Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro
Moshi na Dodoma. Mahakama ya
Hakimu Mkazi mjini Moshi, imeelezwa kuwa marubani wa ndege ya kijeshi ya
Qatar, walitumika katika kutorosha twiga wanne kwenda Uarabuni na
kwamba washtakiwa walikuwa na hati za kusafiria zenye hadhi ya
kidiplomasia.
Shahidi wa 13, Prisca Sabugo ambaye ni Ofisa
Uhamiaji, aliiambia mahakama juzi kuwa hati hizo hazikugongwa mihuri
wala kupewa viza.
Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Kobelo, shahidi huyo alidai kuwa
ndege hiyo ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(Kia) Novemba 24 mwaka 2011.
“Baada ya hiyo ndege ya jeshi kutua, alikuja
wakala wao kutoka Kampuni ya Equity Aviation akaniletea Diplomatic
Passport zao na akaniambia wamekuja kwa shughuli za utalii kwa siku
tatu,” alisema.
Huku akiongozwa na mawakili wa Serikali, Evetha
Mushi na Joseph Maugo, shahidi huyo alidai kuwa marubani na wafanyakazi
wa ndege huwa hawapitii utaratibu wa kawaida wa kujaza fomu na kupewa
viza. Alisema, tangu wageni hao waingie nchini kama watalii, hawakuwahi
kuhojiwa na chombo chochote kuhusu kutogongwa mihuri kwenye hati zao.
Shahidi wa 12, Oscar Jullius ambaye ni Ofisa
Wanyamapori, alidai kuwa vibali vilivyotumika kukamata wanyama hao
vilikuwa vya kampuni mbili ambazo ni Ham Market na Luega Birds Traders.
Kwa mujibu wa shahidi huyo, vibali hivyo vilikuwa
vya kumiliki nyara na si vya kukamata wanyamapori hai na kwamba yeye
ndiye aliyeandika ripoti ya thamani ya wanyama hao.
Alisema thamani ya wanyama wote waliotoroshwa
ilikuwa ni Sh170.5 milioni na kwamba twiga hao wanne kila mmoja alikuwa
na thamani ya Dola 10,000 za Marekani sawa Sh60 milioni za Tanzania.
Alipoulizwa na mmoja wa mawakili wanaowatetea
washtakiwa, Edmund Ngemela, kama vibali walivyokuwa navyo vilikuwa
halali, alikiri kuwa vilikuwa halali na vilikuwa ni vya kumiliki nyara.
Kesi hiyo imepangwa kuendelea Novemba 29 mwaka huu.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni pamoja na raia wa
Pakistan, Kamran Ahmed, Hawa Mang’unyuka, Martin Kimath na Michael Mrutu
ambao wote wako nje kwa dhamana.
Katika hatua nyingine, madiwani watatu wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro akiwamo mwenyekiti wa halmashauri
hiyo, wanashikiliwa na maofisa wa Kikosi cha Maalumu cha Kupambana na
ujangili.
SOURCE : MWANANCHI
Huko Dodoma, watu sita wamekamatwa na polisi wilayani Kondoa
baada ya kupatikana na vipande vinane vya meno ya ndovu yenye thamani ya
Sh 25mil.
ioni.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda,
aliwambia waandishi wa habari jana kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa
katika operesheni maalum ya kupambana na ujangili.
SOURCE : MWANANCHI