Mapiganao yameibuka upya kati ya wanajeshi wa serikali na waasi
kaskazini-mashariki mwa Kongo, zimesema pande mbili na Umoja wa Mataifa,
siku chache baada ya kushindwa kwa ya mazungumzo ya amani mjini
Kampala.
Msemaji wa waasi wa M23 Vianney kazarama alisema mapigano hayo ambayo
yaliwalaazimu maelfu ya raia kuyakimbia makaazi yao, yalitokea umbali wa
kilomita 25 kaskazini mwa Goma, mji muhimu wa wakaazi milioni moja
uliyopo katika eneo lenye utajiri mkubwa wa madini la mashariki, lakini
linalokabiliwa na machafuko ya mara kwa mara.
Rwanda yatishia kujibu mapigo
Nchi jirani ya Rwanda iliwashtumu wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa kurusha makombora matatu ndani ya mipaka yake na kutishia kujibu iwapo mashambulizi yataendelea. Kazarama alisemam jeshi lilishambulia ngome za waasi mapema siku ya Ijumaa, lakini jeshi hilo lilisitiza kuwa lilishambuliwa kwanza -- madai yanayoungwa mkono na duru kutoka ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO.
Nchi jirani ya Rwanda iliwashtumu wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa kurusha makombora matatu ndani ya mipaka yake na kutishia kujibu iwapo mashambulizi yataendelea. Kazarama alisemam jeshi lilishambulia ngome za waasi mapema siku ya Ijumaa, lakini jeshi hilo lilisitiza kuwa lilishambuliwa kwanza -- madai yanayoungwa mkono na duru kutoka ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO.
Taarifa ya MONUSCO, ambayo ilishiriki mapigano hayo sambamba na jeshi la
Kongo, ilisema ghasia ziliendelea kwa siku nzima. MONUSCO ilisema
ilikuwa na wasiwasi mkubw ajuu ya kuanza tena kwa uadui, na kuwatolea
wito waasi wa M23 kurudi kwenye meza ya mazungumzo. "Niko makini katika
juhudi zetu za kuwalinda raia na kuyatangua makundi yote yenye silaha
ili kurejesha amani na utulivu," alisema mkuu wa MONUSCO martin Kobler.
Mkuu wa MONUSCO, Martin Kobler.
Mwanaharakati wa haki za binaadamu katika eneo hilo aliziona helikopta
za Umoja wa Mataifa zikiruka juu ya kijiji cha Kibumba, ambacho ni ngome
ya M23 iliyoshambuliwa, na alisema kuwa raia walikuwa wanakimbia
kuelekea mpaka wa Rwanda.
Baraza ya usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Machi liliidhinisha
kupelekwa kwa kikosi maalumu cha Afrika chenye wanajeshi 3,000 chini ya
MONUSCO, ambacho kinaongozwa na Jenerali kutoka Tanzania, kikiwa na
mamlaka ya kufanya mashambulizi dhidi ya makundi ya waasi nchini Kongo.
Jeshi la Rwanda lilisema kuwa makombora matatu yaliangukia katika ardhi
yake, na kumjeruhi raia. "Kama hawako tayari kusitisha hili, tutajibu
mara moja na itauma," alisema balozi w arwanda katika Umoja wa Mataifa
Eugene Richard Gasana baada ya mazungumzo ya baraza la usalama la Umoja
wa Mataifa kuhusiana na wasiwasi uliyoongezeka. Wizara ya wakimbizi ya
Rwanda ilisema kati ya watu 2,500 na 3,000 wamekimbilia nchini humo
kupitia mipaka miwili.
Hujuma dhidi ya mazungumzo ya amani
Siku ya Jumatatu, makundi hasimu yalitangaza kuwa yanasitisha mazungumzo ya amani yanayofanyika katika mji mkuu wa Uganda Kampala, licha ya shinikizo kutoka kwa Umoja wa Mataifa kukomesha uasi huo wa miaka miwili na nusu unaosababisha uharibufu mkubwa mashariki mwa Kongo.
Siku ya Jumatatu, makundi hasimu yalitangaza kuwa yanasitisha mazungumzo ya amani yanayofanyika katika mji mkuu wa Uganda Kampala, licha ya shinikizo kutoka kwa Umoja wa Mataifa kukomesha uasi huo wa miaka miwili na nusu unaosababisha uharibufu mkubwa mashariki mwa Kongo.
Kwa mujibu wa serikali ya Kongo, mazungumzo hayo yalisitishwa kutoka na
tofauti ju ya msamaha kwa wanajeshi walioasi na kurejeshwa kwao katika
jeshi la taifa. Ikiungwa mkono na jamii ya kimataifa, serikali ya Kongo
inakataa kutoa msamaha kwa karibu viongozi 80 wa kundi la M23, na
kuwarejesha tena katika vyeo vya kijeshi.
Rais Joseph Kabila wa Kongo, na Paul Kagame wa Rwanda.
Katika taarifa siku ya Ijumaa, msemaji wa upande wa kisiasa wa M23 Amani
Kabasha aliituhumu serikali mjini Kinshasa, kwa kuyahujumu jumla
mazungumzo ya amani mjini Kampala. Wengi wa wajumbe wa kundi la M23 ni
Watutsi kutoka kundi la awali la waasi amabo waliingizw akatika jeshi la
taifa mwaka 2009, na baadae kuasi mwaka 2012, wakidai kuwa Kinshasa
ilishindwa kusimamia sehemu yake ya makubaliano.
Waasi walichukuwa udhibiti wa mji wa Goma, ambao ndiyo mji mkuu wa jimbo
la Kivu ya Kaskazini kwa zaidi ya wiki moja mwishoni mwa uliyopita,
kabla ya kujiondoa kutokana na shinikizo la kimataifa. Serikali ya Kongo
kwa muda mrefu imeishtumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi, na wataalamu
wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa kamandi ya kundi la M23, iliongozwa
na waziri wa ulinzi wa Rwanda.
Mwanaharakati wa haki za binaadamu alisema kuwa katika eneo la Kabagana,
karibu na mpaka wa Rwanda, aliwaona wanajeshi wa Rwanda wakiingia
kuwasaidia M23. Kigali imekanusha vikali tuhuma kwamba ilikuwa
inawapatia silaha na kuwafadhili waasi -- na hata kuwasaidia kwa kutumia
vikosi vyake yenyewe.
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/afpe
Mhariri: Sekione Kitojo
Mhariri: Sekione Kitojo
SOURCE: DW