Na Fidelis Butahe,
Posted Jumanne,Oktoba1 2013 saa 24:0 AM
Posted Jumanne,Oktoba1 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi
za Chadema leo, Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura
alisema haiwezekani kwa Serikali kuwa mlalamikaji, mtetezi na jaji.
Dar es Salaam. Umoja wa vyama vitatu vya
Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi vimesema Serikali haikufuata taratibu
kufungia kuchapishwa kwa Magazeti ya Mwananchi na Mtanzania.
Viongozi wa kamati ya pamoja ya vyama hivyo,
wamesema kuwa Serikali haikutenda haki kwa kuyafungia magazeti hayo
badala yake, ilitakiwa kuwasilisha malalamiko yake Baraza la Habari
Tanzania (MCT).
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za
Chadema leo, Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura
alisema haiwezekani kwa Serikali kuwa mlalamikaji, mtetezi na jaji.
Sungura alisema alikutana kwa saa mbili na
viongozi wa vyama hivyo; John Mnyika (Chadema) na Abdul Kambaya (CUF)
kujadili suala hilo.
Alisema watu wangependa kujua mtu aliyelalamikia
habari zilizoandikwa na magazeti hayo… “Tunataka kujua kwa nini Serikali
haikupeleka malalamiko yake MCT?”
Maandamano ya nchi nzima palepale
Sungura alisema pia kuwa vyama vyao vitatu
vinaendelea na maandalizi ya maandamano ya nchi nzima yatakayofanyika
Oktoba 10, mwaka huu.
Maandamano hayo yana lengo la kumshinikiza Rais
Jakaya Kikwete asisaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013.
Sungura alisema kuwa maandamano hayo yataandaliwa kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI