Na Herieth Makwetta, Mwananchi
Posted Septemba21 2013 saa 10:17 AM
Posted Septemba21 2013 saa 10:17 AM
Kwa ufupi
Mshindi wa taji hilo mwaka huu atajinyakulia gari
jipya na kitita cha fedha Ssh 8milioni kutoka kwa wadhamini wakuu wa
mashindano hayo, Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL).
Dar es Salaam.: Mrithi wa Redds Miss Tanzania
2013, Brigiter Alfred atapatikana leo wakati warembo 30 watakapopanda
jukwaani kwenye Uukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Mshindi wa taji hilo mwaka huu atajinyakulia gari
jipya na kitita cha fedha Ssh 8milioni kutoka kwa wadhamini wakuu wa
mashindano hayo, Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL).
Akizungumza jana Mkurugenzi wa Lino Agency ambao
ndiyo waandaaji wa mashindano hayo, Hasheem Lundenga alisema taji la
malkia mpya wa urembo Tanzania limeshaandaliwa na mshindi wa pili mwaka
jana ndiye atakayemvisha mshindi.
“Redds Miss Tanzania 2012 namba mbili, Eugene
Fabian ndiye atakayemvisha taji malkia mpya baada ya Miss Tanzania 2012
Brigiter Alfred anayemaliza muda wake kuwaepo Indonesia akijiandaa
kuwania taji la Miss World mwaka huu hapo Septemba 28,” alisema.
Kwa hivi sasa, taji la Redd’s Miss Tanzania
linashikiliwa na Miss Sinza, Brigiter Alfred, aliyelitwaa taji hilo
mwaka jana na kukabidhiwa gari aina ya Noah na kitita cha Ssh milioni
nane.
Mshindi wa taji la mwaka huu atakuwa wa 21 katika
historia ya mashindano ya urembo nchini na ataiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya dunia ya mwakani.
Meneja wa Redds Original, Victoria Kimaro alisema
kuwa siri kubwa ya kuingiza fedha katika mashindano hayo ni kuchangia
maendeleo ya sanaa nchini, kuwawezesha wasichana wadogo, kuvumbua vipaji
mbalimbali vya kujitangaza kibiashara.
Mashindano hayo yamepangwa kuanza saa 2 usiku na
yatapambwa na burudani za kila aina kutoka kwa wasanii maarufu wa ndani
na nje. Wasanii hao ni Judith Wambura “ Lady Jaydee” na msanii wa kizazi
kipya kutoka Uganda, Mike Ross.
Mshindi wa pili atapata sh 6.2milioni , wa tatu sh
4milioni, wa nne sh3 milioni, wa tano sh 2milioni, huku mshindi wa sita
hadi 15 watapata sh 1.2milioni kila mmoja na waliobaki watajipoza kwa
sh 700,000 kila mmoja.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI