Na Mwandishi Wetu na Mashirika ya Umma
Posted Septemba28 2013 saa 8:23 AM
Posted Septemba28 2013 saa 8:23 AM
Kwa ufupi
Wanamageuzi hao kupitia kundi lao lenye vikundi
vidogo 100 vya Wakatoliki wanataka suala lao liwe sehemu ya mazungumzo
baina ya Papa Francis na kamati yake ya ushauri yenye makadinali wanane
yanayofanyika wiki ijayo.
Paris, Ufaransa. Harakati za kutaka mabadiliko
makubwa ndani ya Kanisa Katoliki zimezidi kushika kasi baada ya kundi la
waumini wanaojiita wanamageuzi kumwandikia barua Papa Francis, wakiomba
akutane nao kuzungmzia mustakabali wa kanisa hilo.
Wanamageuzi hao kupitia kundi lao lenye vikundi
vidogo 100 vya Wakatoliki wanataka suala lao liwe sehemu ya mazungumzo
baina ya Papa Francis na kamati yake ya ushauri yenye makadinali wanane
yanayofanyika wiki ijayo.
Papa Francis anatarajiwa kukutana na makadinali
hao wanaounda Baraza la Ushauri kati ya Oktoba 1-2 mjini Vatican kwa
lengo la kuangalia mageuzi katika uendeshaji wa kanisa hilo.
Hadi sasa, haijulikani endapo Papa Francis ataafiki ushauri wa wanamageuzi hao au la.
Katika mkutano huo, Papa Francis na bodi yake
wanatazamiwa kuangalia sera mbalimbali zinazohusu uendeshaji wa kanisa
hilo. Makadinali hao wanane wanatoka Italia,Chile,India,Ujerumani,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Marekani, Australia na Honduras.
Msemaji wa kundi hilo la wanamageuzi kutoka
mataifa mbalimbali duniani, Rene Reid ameeleza kuwa matumaini yao ni kwa
kiongozi huyo wa kanisa kukubali kukutana nao.
Kundi hilo lina Wakatoliki kutoka nchi mbalimbali
zinazozungumza Kiingereza pamoja na Ujerumani, Austria, Ufaransa,
Poland, Hispania na India.
Barua hiyo inaorodhesha mambo ambayo Papa Francis
aliyechaguliwa Machi amekuwa akitaka yafanyiwe marekebisho na mengine
ambayo tayari amepingana nayo.
Katika mahojiano mbalimbali wiki iliyopita, Papa
Francis amezungumzia mambo ambayo angependa yafanyiwe marekebisho na
kanisa,ingawa siyo yale yanayohusu mafundisho na kumsihi aishi kwa
matendo ahadi zake.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI