Na Salim Mohammed
Posted Jumatatu,Septemba30 2013 saa 24:0 AM
Posted Jumatatu,Septemba30 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Hamad aliisifu Serikali ya Kikwete kwa
kuwaachia wananchi wenyewe kuiandika katiba yao na kumwomba asikubali
kutia saini muswada huo wa sheria.
Tanga. Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad
amesema mgogoro wa Muungano uliopo unatokana na kufichwa kwa makubaliano
yaliyowekwa na waasisi wa Muungano na kusema kero hizo hazitakwisha
hadi kutakapoundwa Serikali tatu na Muungano wa mkataba.
Alisema hayo juzi wakati wa kongamano la
Wazanzibar waishio Bara na kusema Muungano uliotiwa saini na waasisi wa
Muungano huo umefichwa na kusema dawa yake ni Serikali tatu na Muungano
wa mkataba.
Hamad ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar, alimtaka Rais Jakaya Kikwete kutosaini Muswada wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013 kwa maelezo kuwa una
kasoro.
“Wazanzibari wenzangu na mimi pia ni mmoja wao
ambao tunataka Muungano wa mkataba, nilipoulizwa na tume nilisema nataka
Muungano wa mkataba nadhani nanyi pia mawazo yenu ni kama mimi,”
alisema Hamad.
Hamad aliisifu Serikali ya Kikwete kwa kuwaachia
wananchi wenyewe kuiandika katiba yao na kumwomba asikubali kutia saini
muswada huo wa sheria.
Alisema Zanzibar ni nchi kamili yenye mamlaka kama
ilivyo kwa nchi nyingine hivyo inahitaji kurejeshewa mamlaka yake na
kuwa na uamuzi ikiwa na pamoja kurejeshewa kiti chake katika Baraza la
Umoja wa Kimataifa.
“Zanzibar iko na haki ya kuingia mikataba na
jumuiya za kimataifa kama ilivyo nchi nyingine, tunataka dola ya
Zanzibar iliyo nchi kamili kama ilivyokuwa zamani, Muungano umeifuta
Zanzibar katika ramani ya kimataifa,” alisema na kuongeza:
“Hivi sasa Zanzibar haina haki ya kusema inajiunga
na jumuiya yoyote ya kimataifa, kikwazo hiki ni kufichika kwa
makubaliano ya Muungano kutoka kwa waasisi wetu."
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI