29th September 2013
Kampuni
ya kuhudumia ndege, abiria na mizigo Swissport kwa kushirikiana na
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini wamejipanga kuzuia ugaidi kuingia
nchini.
Mkurugenzi wa Swissport, Gaudency Temu,
aliwaambia wanahabari waliofanya ziara katika viwanja mbali mbali vya
ndege nchini sambamba na uwekaji wa mashine mpya na za kisasa
zilizonunuliwa na Swissport kwa lengo la kupunguza uhalifu nchini.
Katika zirara hiyo baadhi ya wanahabari
wameshuhudia mtambo mpya wa kuzuia uhalifu ikifanya kazi kwa kuongezwa
na wataalam ambao wamepata mafunzo nchini Israel.
Mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha kupakia
na kupokea mizigo Swissport Cargo, Oscar Mgina, alisema kutokana na
kufungwa kwa mashine mpya na za kisasa katika kitengo hicho, Swissport
imekuwa mwiba mkali kwa watu wasio waaminifu ambao wamekuwa
wakisafirisha maliasili na madini kinyume na taratibu za mamlaka husika.
CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI