Na Herieth Makwetta, Mwananchi
Posted Septemba28 2013 saa 24:0 AM
Posted Septemba28 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Warembo walilicheza kwa ubunifu licha ya
wachache wao kukosea na kujichanganya. Katika shoo warembo hao walivalia
mavazi tofauti huku wakiiga uchezaji wa Kundi la P Sqare wakichanganya
na uchezaji wa wimbo wa Thriller ulioimbwa na hayati Michael Jackson.
Dar es Salaam. Suti nyeusi
yenye shati nyeupe na tai nyekundu kwa wanaume na magauni marefu na
mafupi kwa wanawake, ndiyo mavazi yaliyotawala usiku wa kumtafuta malkia
mpya wa urembo nchini Tanzania Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Kila mgeni aliyewasili kwa lengo la kuingia
ukumbini humo alihitajika kupita katika zulia jekundu ‘red carpet’ kwa
ajili ya mahojiano mafupi na mtangazaji Sauda Mwilima wa Star Tv pia
kupiga picha, kabla ya kuingia kupitia milango miwili wa VIP na ule wa
viti vya kawaida.
Onyesho lilianza saa 3 usiku likifunguliwa na shoo
ya warembo wote 30 waliocheza dansi kupitia wimbo wa ‘Personally’ wa
wasanii P Sqare, dansi walilofunzwa na msanii wa ngoma za asili Wanne
Star.
Warembo walilicheza kwa ubunifu licha ya wachache
wao kukosea na kujichanganya. Katika shoo warembo hao walivalia mavazi
tofauti huku wakiiga uchezaji wa Kundi la P Sqare wakichanganya na
uchezaji wa wimbo wa Thriller ulioimbwa na hayati Michael Jackson.
Kikundi cha ngoma za asili cha Mama Afrika ndicho
kilichoendeleza burudani katika Jukwaa la Redds Miss Tanzania lililokuwa
na upana na hadhi ya aina yake ambapo baadaye warembo waliingia na
mavazi ya ubunifu yaliyobuniwa na wabunifu mbalimbali wa hapa nchini.
Wakati wa kuonyesha vazi la ubunifu warembo
walitambulishwa kwa majina yao na hadhi zao kwa makundi, kisha kupanda
jukwaani ikishuhudiwa jitihada za wabunifu zilizoonyesha uwezo wao kwa
kubuni mavazi mapya machoni pa wengi.
Baada ya kuonyesha vazi la ubunifu, warembo
walirejea jukwaani safari hii wakionyesha vazi la ufukweni,
lililonakshiwa na kitenge cha Kiafrika ambalo ni ubunifu wa Veronica
Lugenzi. Jambo la kushangaza lililojitokeza ni vazi hilo kuvaliwa na
viatu virefu, badala ya viatu vifupi vya wazi kama ilivyo uhalisia wa
vazi la ufukweli, kosa linalojirudia kwa miaka kadhaa sasa.
Kuhitimishwa kwa onyesho la vazi la ufukweni
kulitoa fursa kwa jukwaa kupambwa na burudani ya muziki iliyotolewa na
mwanamuziki Judith Wambura maarufu Lady JD aliyevaa vazi
lililopendezeshwa na mchanganyiko wa rangi nyeusi, dhahabu na fedha. Akiongozwa na Dj Choka, Lady JD aliimba wimbo unaotambulika kwa jila la Wangu aliomshirikisha Mr Blue, kisha kuimba wimbo maarufu wa Joto Hasira kabla ya kushuka jukwaani na kuwapisha warembo, waliopanda na vazi la jioni.
lililopendezeshwa na mchanganyiko wa rangi nyeusi, dhahabu na fedha. Akiongozwa na Dj Choka, Lady JD aliimba wimbo unaotambulika kwa jila la Wangu aliomshirikisha Mr Blue, kisha kuimba wimbo maarufu wa Joto Hasira kabla ya kushuka jukwaani na kuwapisha warembo, waliopanda na vazi la jioni.
Licha ya awali kutangazwa kwamba mwanamuzi huyo
angekuwa na bendi yake, lakini hali ilikuwa tofauti kwani aliimba kwa
‘play back’ jambo lililowashangaza wengi.
Kimbwanga kiliibuka pale mrembo mmoja aliyekuwa
amevalia nambari 6 kujikuta gauni alilovaa likizuiwa na kiatu kisha
kujikwaa kwenye ngazi alipotaka kupanda jukwaani kutoka nyuma ya jukwaa.
Mrembo huyo alijaribu kujinasua zaidi ya mara tatu na kushindwa hivyo
kuamua kurudi nyuma ya jukwaa, kabla ya kupanda tena jukwaani na kundi
lililofuata huku akionekana kukosa kujiamini tofauti na alivyokuwa
awali.
Baada ya warembo kuonyesha mavazi hayo walichaguliwa walioinga 15 bora sanjari na warembo watano walioshinda mataji mbalimbali.
Mwanamuziki Mike Ross kutoka Uganda ndiye
aliyepokea jukwaa na kutoa burudani kabla ya kumpisha Lady JD aliyepanda
kwa mara ya pili na kuuinua umati wa mashabiki kwa kuimba wimbo wake
unaotamba zaidi kwa sasa ‘Yahaya’ kabla ya kumpisha jaji kusoma majina
ya warembo watano walioingia hatua ya fainali.
Jaji huyo, Dk Ramesh Shaa alisoma majina ya warembo walioingia
hatua ya fainali ambao ni Lucy Tomeka, Isabel Petty, Clara Bayo, Latifa
Mohamed na Happiness Watimanywa.
Warembo hao waliulizwa maswali mbalimbali
waliyoyachagua, wa kwanza kuchagua swali akiwa Happiness Watimanywa
aliyechagua swali namba tano lilimhoji iwapo atachaguliwa kuwa Miss
Tanzania atafanya kipi ambacho warembo waliotangulia walishindwa kufanya
katika nyanja tofauti. Happyness alijibu swali hilo kwa ufasaha na
umakini mkubwa hali iliyoufanya ukumbi ulipuke kwa shangwe.
Katika mashindano hayo ambayo kwa miaka miwili
sasa yanadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s, Happiness Watimanywa, ndiye
aliyeibuka kuwa malkia mpya wa urembo na kuvikwa taji la Redds Miss
Tanzania, akiandika historia mpya katika miaka 21 ya mashindano hayo.
Happiness mwenye umri wa miaka 19, aliyeibukia
kutoka mashindano ya urembo ngazi za vitongoji mkoani Dodoma, anakuwa
mshindi wa kwanza aliyekubalika vilivyo na wapenzi wa fani ya urembo
nchini sanjari na warembo wenzake 29 aliokuwa akichuana nao.
Nafasi ya pili ilikwenda kwa Latifa Mohamed huku
nafasi ya tatu ikichukuliwa na Clara Bayo. Nafasi ya nne na tano
zilikwenda kwa Isabel Petty na Lucy Tomeka.
Taji lililoongezeka usiku huo ni la Balozi wa Marie Stopes, ambalo lilikwenda kwa Marietha Boniphace.
Wasifu wa Happyness Watimanywa
Happiness Watimanywa, ndiye msichana pekee kutoka
Tanzania aliyeweka historia ya kuongoza nchi zaidi ya 150 za mtandao wa
IGCSE katika somo la Uhasibu kwenye mitihani ya Kidato cha Nne mwaka
2010.
Yeye ni mzaliwa wa familia ya Louis Roussos ya
Morogoro. Wadogo zake Angel na Romeo sasa wanasoma
shule ya St Constantine ya mkoani Arusha ambayo pia alisoma malkia
huyo. Happiness amewahi kusoma Laureatte International School ya Dar es
Salaam, ambapo alikutana na mwalimu wa michezo anayemtaja kwa jina la
Tchalewa Ndeki akimwelezea kuwa ndiye aliyemfungulia mipaka ya
kimataifa.
Akiwa Laureatte, Happiness aliwahi kwenda China na
South Korea pamoja na wanafunzi wenzake katika matamasha mbalimbali ya
elimu na michezo. Baada ya kumaliza kidato cha nne, alifanikiwa kujiunga
na Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Uingereza anaposomea Shahada ya
Biashara.
Kipindi Happiness alipokuwa kwenye likizo ndefu,
aliamua kujihusisha na masuala ya urembo na kufanikiwa kutwaa Taji la
Miss Dodoma, Miss Kanda ya Kati na hatimaye kuingia kwenye Kambi ya Miss
Tanzania.
SOURCE: MWANANCHI
Akiwa Miss Tanzania, Happiness alikuwa ni mshiriki wa kwanza
kuingia nusu fainali ya mashindano hayo kwa kutwaa taji la Redds Miss
Photogenic 2013.
Ndani ya Kambi ya Miss Tanzania, Happiness
Watimanywa alikuwa mwiba kwa warembo wengine 29 wanaowania taji hilo
kwani alikuwa akionyesha uwezo wa hali ya juu kuanzia kwenye kipaji hata
michezo, mbali na upeo mkubwa alio nao.
Akizungumzia Redd’s Miss Tanzania, Happeness
alisema kwa kifupi: “Nilipoingia kambini nilipata hofu kuona warembo
wenzangu, wengi walikuwa wazuri pia wenye uwezo, nikajitahidi kuwa
karibu nao kuondoa hofu na kujenga kujiamini zaidi kuwa naweza.”
SOURCE: MWANANCHI