Na Nairobi,Kenya
Posted Jumatatu,Septemba30 2013 saa 10:52 AM
Posted Jumatatu,Septemba30 2013 saa 10:52 AM
Kwa ufupi
Kitendo hicho kilipokelewa kwa hisia tofauti na
Serikali ya Kenya kwa kudai kwamba hatua hiyo iliyochukuliwa na
Marekani sio sahihi.
Baada ya magaidi kuvamia kituo cha biashara cha
Westgate nchini Kenya wiki iliyopita ,Marekani imetoa onyo kwa raia
wake kuacha kusafiri kuelekea nchini humo.
Kitendo hicho kilipokelewa kwa hisia tofauti na
Serikali ya Kenya kwa kudai kwamba hatua hiyo iliyochukuliwa na
Marekani sio sahihi.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Wizara ya
Mambo ya Nje ya Kenya ililaani vikali hatua ya Marekani ya kuwaonya raia
wake kufanya safari nchini Kenya.
Taarifa hiyo iliitaja hatua hiyo kuwa, haina umuhimu na pia ilitolewa katika wakati ambao sio mwafaka.
Ripoti hiyo iliongeza kuwa, shambulizi la Westgate
jijini Nairobi, ni tatizo la ulimwengu mzima hasa kwa kuzingatia kuwa,
hata Marekani yenyewe imekwishaathiriwa na vitendo kama hivyo vya
kigaidi.SOURCE: MWANANCHI