Kwa ufupi
Alisema haoni uwezekano wa Dk Mwakyembe
kufanikiwa katika mapambano hayo, kwani hata kama viwanja vya ndege
vitafungwa mashine za kubaini waliobeba dawa hizo, kama wasimamiaji
watapokea rushwa hakuna atakayekamatwa.
Dar es Salaam. Jaji mstaafu wa Mahakama ya
Rufaa, Thomas Mihayo amesema kushamiri kwa matukio ya uuzwaji, ununuaji
wa dawa za kulevya, sambamba na upitishaji wa dawa hizo katika viwanja
mbalimbali vya ndege nchini, kunachangiwa na rushwa iliyokithiri katika
Mahakama na Polisi.
Amesema matukio mengi ya mauaji ya raia wasio na
hatia pamoja na upitishwaji wa wanyamapori (Twiga) katika viwanja vya
ndege mbalimbali nchini hayachukuliwi hatua stahiki kwasababu rushwa
imetawala, “Kuzungumzia rushwa siyo hoja, tatizo ni kuwa matendo yetu ni
tofauti na kauli tunazotoa.” Katika maelezo yake alisema anamuonea
huruma Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, kwani licha ya
kuonyesha wazi kutaka kupambana na watu wanaoingiza dawa za kulevya
kupitia katika viwanja vya ndege, hataweza kwa maelezo kuwa rushwa ndiyo
inafanikisha mipango yote ya uingizwaji wa dawa hizo.
Jaji Mihayo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) aliyasema hayo jana katika
mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili, huku akitoa mifano ya kesi
mbalimbali ambazo watuhumiwa waliachiwa huru katika mazingira
yanayoonekana wazi kuwa Mahakimu walipewa rushwa.
“Twiga kusafirishwa kupitia viwanja vya ndege
maana yake ni rushwa ilitembea na siyo uzembe. Sasa tunaona mauaji ya
watu wasio na hatia lakini vyombo vya dola vinafumba macho na hakuna
kinachofanyika.Katika nchi inayofuata sheria mambo kama haya lazima
yafanyiwe kazi, lakini ukiona kimya maana yake rushwa imetawala” alisema
na kuongeza;
“Rushwa imetoka huko sasa imeingia katika dawa za
kulevya, Watanzania wengi wanadhani dawa za kulevya kupita katika uwanja
wa ndege ni uzembe wa wasimamizi, hilo siyo kweli yamepita kwa sababu
ya rushwa.”
“Hawa watu polisi wanawajua lakini wanawalinda…, ndiyo wanalindwa na haohao polisi” alisisitiza.
Akitolea mfano tukio la Julai 5 mwaka huu la
upitishaji wa mabegi tisa ya dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) lililoanikwa na hadharani na
Dk Mwakyembe, ambapo watu mbalimbali walitajwa kuhusika, wakiwemo
maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa ambao walidaiwa kuchelewesha mbwa
kwa ajili ya kukagua mizigo alisema, “Mbwa hawawezi kupokea rushwa na
kama wangekuwepo katika uwanja wa ndege. Ni wazi kuwa wangeweza kubaini
dawa hizo za kulevya.”
Alifafanua, “Dk Mwakyembe alieleza wazi kuwa mbwa
walichelewa kufika uwanja wa ndege, swali la kujiuliza kwa nini
walichelewa? Sababu za kuwachelewesha zinaweza kuwa nyingi tu, unaweza
kusema gari liliharibika.”
Alisema haoni uwezekano wa Dk Mwakyembe kufanikiwa
katika mapambano hayo, kwani hata kama viwanja vya ndege vitafungwa
mashine za kubaini waliobeba dawa hizo, kama wasimamiaji watapokea
rushwa hakuna atakayekamatwa.
“Kama kutakuwa na sheria kali za kudhibiti dawa za
kulevya basi watekelezaji wa sheria hizo wanatakiwa kuwa waaminifu na
kuichukia rushwa. Pia tunaweza kuwa na sheria kali lakini ndiyo rushwa
ikaongezeka zaidi” alisema Jaji Mihayo
“Watanzania watafanikiwa kuikomesha rushwa kama
wakiichukia. Nasema hivi kwa sababu siku hizi mtu aliyekithiri kwa
kupokea rushwa anashabikiwa na wenzake. Mahakama zetu nazo zinatakiwa
zitekeleze wajibu wake ipasavyo” alisema
SOURCE: Mwananchi
SOURCE: Mwananchi
Dar
es Salaam. Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Thomas Mihayo amesema
kushamiri kwa matukio ya uuzwaji, ununuaji wa dawa za kulevya, sambamba
na upitishaji wa dawa hizo katika viwanja mbalimbali vya ndege nchini,
kunachangiwa na rushwa iliyokithiri katika Mahakama na Polisi.
Amesema matukio mengi ya mauaji ya raia wasio na
hatia pamoja na upitishwaji wa wanyamapori (Twiga) katika viwanja vya
ndege mbalimbali nchini hayachukuliwi hatua stahiki kwasababu rushwa
imetawala, “Kuzungumzia rushwa siyo hoja, tatizo ni kuwa matendo yetu ni
tofauti na kauli tunazotoa.” Katika maelezo yake alisema anamuonea
huruma Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, kwani licha ya
kuonyesha wazi kutaka kupambana na watu wanaoingiza dawa za kulevya
kupitia katika viwanja vya ndege, hataweza kwa maelezo kuwa rushwa ndiyo
inafanikisha mipango yote ya uingizwaji wa dawa hizo.
Jaji Mihayo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) aliyasema hayo jana katika
mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili, huku akitoa mifano ya kesi
mbalimbali ambazo watuhumiwa waliachiwa huru katika mazingira
yanayoonekana wazi kuwa Mahakimu walipewa rushwa.
“Twiga kusafirishwa kupitia viwanja vya ndege
maana yake ni rushwa ilitembea na siyo uzembe. Sasa tunaona mauaji ya
watu wasio na hatia lakini vyombo vya dola vinafumba macho na hakuna
kinachofanyika.Katika nchi inayofuata sheria mambo kama haya lazima
yafanyiwe kazi, lakini ukiona kimya maana yake rushwa imetawala” alisema
na kuongeza;
“Rushwa imetoka huko sasa imeingia katika dawa za
kulevya, Watanzania wengi wanadhani dawa za kulevya kupita katika uwanja
wa ndege ni uzembe wa wasimamizi, hilo siyo kweli yamepita kwa sababu
ya rushwa.”
“Hawa watu polisi wanawajua lakini wanawalinda…, ndiyo wanalindwa na haohao polisi” alisisitiza.
Akitolea mfano tukio la Julai 5 mwaka huu la
upitishaji wa mabegi tisa ya dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) lililoanikwa na hadharani na
Dk Mwakyembe, ambapo watu mbalimbali walitajwa kuhusika, wakiwemo
maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa ambao walidaiwa kuchelewesha mbwa
kwa ajili ya kukagua mizigo alisema, “Mbwa hawawezi kupokea rushwa na
kama wangekuwepo katika uwanja wa ndege. Ni wazi kuwa wangeweza kubaini
dawa hizo za kulevya.”
Alifafanua, “Dk Mwakyembe alieleza wazi kuwa mbwa
walichelewa kufika uwanja wa ndege, swali la kujiuliza kwa nini
walichelewa? Sababu za kuwachelewesha zinaweza kuwa nyingi tu, unaweza
kusema gari liliharibika.”
Alisema haoni uwezekano wa Dk Mwakyembe kufanikiwa
katika mapambano hayo, kwani hata kama viwanja vya ndege vitafungwa
mashine za kubaini waliobeba dawa hizo, kama wasimamiaji watapokea
rushwa hakuna atakayekamatwa.
“Kama kutakuwa na sheria kali za kudhibiti dawa za
kulevya basi watekelezaji wa sheria hizo wanatakiwa kuwa waaminifu na
kuichukia rushwa. Pia tunaweza kuwa na sheria kali lakini ndiyo rushwa
ikaongezeka zaidi” alisema Jaji Mihayo
“Watanzania watafanikiwa kuikomesha rushwa kama
wakiichukia. Nasema hivi kwa sababu siku hizi mtu aliyekithiri kwa
kupokea rushwa anashabikiwa na wenzake. Mahakama zetu nazo zinatakiwa
zitekeleze wajibu wake ipasavyo” alisema
- Riadha Taifa yafikia kilele Moro
- Wachezaji 37 pingamizi TFF
- Kiluvya Utd, Villa hapatoshi Kinesi leo
- Mambo mbele kwa mbele
- Yanga yatikisa, Simba yabanwa
- Arsenal yaitupia tatu Fulham
- Hongera Nchimbi, lakini kazi bado mbichi!
- Wanawake 300 waungana Dar
- Biashara ya Dawasco yadaiwa kusababisha kero Kibamba Dar
- Waandamana kupiga vita ujangili
- Ndege ya Rais yadaiwa kubebea mkaa
- Kamati Kuu yamzuia Kagasheki kushiriki siasa mkoani Kagera
- Kanisa lachomwa moto Dar
- Mchakato wa kumrejesha Alex Massawe waiva
- Mansour: Naiachia CCM kunivua uanachama
- Luteni Kanali wa JWTZ atoroka na nyaraka
- Kagame, kujenga nchi miaka kuibomoa dakika
- Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili
- Homa ya ini ni ugonjwa hatari kuliko Ukimwi
- Yanga yatikisa, Simba yabanwa