Thursday, 12 September 2013

Taarifa ya Polisi Pwani: Ajali ya boti yaua; Mnazi mkavu waua; Ajeruhiwa kwa risasi


12/09/2013

 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE

11/09/2013

Kujeruhi kwa risasi: - Tarehe 10/09/2013, saa 6:30 mchana  huko Kijiji Tondoroni (W) Kisarawe (M) Pwani. Omary S/o Mohamed, umri miaka 47, fundi ujenzi, mkazi wa Tondoroni Kisarawe alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni wa kulia na watu wanaosadikiwa kuwa ni askari wa JWTZ kikosi 83 Kiluvya wakati akiendelea na shughuli zake za ujenzi. Chanzo ni madai ya mlalamikaji kujenga katika eneo linalodaiwa ni la Jeshi.

Taarifa ya Kifo. Tarehe 10/09/2013 majira ya 01:20 usiku huko Mbegani katika bahari ya Hindi Kata ya
Zinga (W) Bagamoyo (M) Pwani Watu wapatao sita wakiwa wanasafiri na Boti ijulikanayo kwa jina la GOGO WATER BOAT mali ya Lazy Lagon Lodge wakitokea Mbegani wakielekea kwenye Kisiwa  Las Lagon walizama majini na kusababisha vifo kwa (1) Elikulano S/o Malile, 39 yrs, mlinzi wa hoteli hiyo  na (2) Mwanahawa D/o Mtungi, 30 yrs, mkulima watu wawili walifanikiwa kuopolewa ambao ni Levina S/o Mdemu, 29 yrs,  nahodha wa Boti na (2)  Daudi S/o Kiando, 32 yrs, Fundi injini  na mfanyakazi wa hoteli hiyo,    ambao hawajapatikana  ni (1) Robert S/o Kambo, 34 yrs,  Kapteni wa Boti, (2) Elisando S/o Malile, miezi minne (4) , mtoto wa Mwanahawa  D/o Mtungi. Chanzo cha ni kuchafuka kwa bahari. Juhudi za kuwatafuta waliozama bado zinaendelea.

Taarifa ya kifo: - Tarehe 10/09/2013, saa 10:10 jioni katika Kijiji cha Kiromo (W) Bagamoyo (M) Pwani. Mohamed Iddi umri miaka 9, mkazi wa Kiromo Miono aliangukiwa na mnazi uliokuwa umekauka kichwani na kupasuka fuvu la kichwa wakati wakiwa machungani na wenzake na kufariki papo hapo. Mnazi huo ulikuwa umekauka na mizizi yake kuoza hivyo upepo ulipovuma ndipo ukadondoka na kumwangukia marehemu. Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu kwa mazishi.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA PWANI