Sunday 22 September 2013

Maelfu wajitokeza mkutano wa Chadema,NCCR Mageuzi na Cuf Jangwani


 Maelfu  wakazi wa jiji la Dar es salaam  wengi wao wakiwa ni  wafuasi wa vyama vya Chadema ,Cuf na NCCR Mageuzi  wemefurika katika  viwanja vya jangwani kuwasilikza  viongozi wakuu wa vyama hivyo ambapo kwa pamoja viongozi hao  wanapinga  hatua  ya serikali  kuingiza baadhi ya vipengele  katika mswada wa  sheria  yamarekebishoa  ya  sheria  ya mabadiliko ya katiba vipengele wanavyodai kuwa vitapelekea kupatikana kwa katiba  ya upande moja  na kuongeza kuwa kama mswada huo hautafanyiwa marekebisho  hawatashiriki katika bunge la katiba.
Katika viwanja hivyo  ulinzi uliimarishwa kutoka katika vikundi mbalimbali  vinavyomilikiwa na vyama hivyo  huku shamra shamra za huko na kule zikiwa hazikosekani ili mradi kunogesha mkutano.
Mwenyekiti wa taifa wa Chadema  na ambaye  ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Mh Freeman Mbowe amewataka watanzania kuacha uoga na wasimame imara kudai katiba bora.
Naye mwenyekiti wa Cuf Mh Profesa Ibrahim Lipumba  amesema Tanzani inahitaji katiba ambayo italinda na kusimamia rasilimali za taifa  kuweza kutmia kwa usawa na kuzingatia mahitaji ya watanzania wenyewe.
Kwa upande wake mwenyekiti wa NCCR Mageuzi  na mbuge wa kuteuliwa amesema hakun haja ya kutumi mabavu  na badala yake ameitaka serikali itumiye busara zaidi ili kuweza kufiki mwafaka wa jambo hili.