Friday, 23 August 2013

Dk Susan Mboya-Kidero kuongoza Coca-Cola Afrika

Na Mwandishi Wetu  (email the author)

Posted  Alhamisi,Agosti22  2013  saa 20:39 PM
Kwa ufupi
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari juzi, ilisema kuwa kazi yake itakuwa kufuatilia kazi za taasisi hiyo Kaskazini, Magharibi, Kusini, Mashariki na Afrika ya Kati pamoja na kuongoza mipango ya mradi ya kimaendeleo na kiutekelezaji ya TCCAF.

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Coca-Cola Group wa Uwezeshaji wa Wanawake Kiuchumi wa Eurasia na Afrika (Women’s Economic Empowerment for Eurasia & Africa), Dk Susan Mboya-Kidero ameteuliwa kuwa Rais wa The Coca-Cola Africa Foundation (TCCAF).
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari juzi, ilisema kuwa kazi yake itakuwa kufuatilia kazi za taasisi hiyo Kaskazini, Magharibi, Kusini, Mashariki na Afrika ya Kati pamoja na kuongoza mipango ya mradi ya kimaendeleo na kiutekelezaji ya TCCAF.
Dk Mboya-Kidero alijiunga na Kampuni ya Coca-Cola Septemba 2008 kama Meneja Mkuu wa Franchise na Coca-Cola Canners wa Afrika Kusini. Alipandishwa cheo kuwa Mkurugenzi wa Coca-Cola Group wa Uwezeshaji wa Wanawake milioni tano kiuchumi ifikapo 2020 (5By20).
Aliongoza juhudi za kikundi cha kuchangia fedha kikamilifu kuelekea dhamira ya kampuni ya kimataifa ya kuwawezesha wanawake wajasiriamali wa Coca-Cola value chain 2020.
Alifanikisha haya kwa kufanya kazi kwa mfumo wa Afrika, India, Mashariki ya Kati, Uturuki na Urusi ili kuboresha maendeleo endelevu ya biashara ndogo ndogo,.
Ni mwanamke anayetajwa kutoa nafasi za kazi nyingi na uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake katika nafasi za ujasiriamali ndani ya Coca-Cola value chain.